Bukobawadau

HAPA NA PALE NA CAMERA YETU MAY 14,2014

Kama kawaida mwanalibeneke wenu katika hapa na pale ,nimekuwa napenda kufika sehemu mbalimbali,iwe kiangazi au masika , Iwe mchana ama Usiku kwa lengo la kukufikihia kila kinachojili 
 Nafika Kiwanja cha New Coffee Tree Hotel ,kiwanja kinachopendwa na watu wengi kutokana na ubora wa hutuma zake.
 Nakutana na kijana Hasheem Omary Said maarufu kama 'Hasheem Dalali' akiwa ndani ya vazi la maalum la kitenge,tunasema 'kikwetu kwetu' au 'Sambaza upendo Tanzania at 50
 Akiwa na mwanadada Vannessa,Inanilazimu kutoa nafasi kubwa, kufuatia kupendeza kwao kiasili kwa kuvaa vazi la kitenge,Ni vazi lililokuwa linavaliwa sana makanisani, ama kufungwa tu mtu akiwa nyumbani au kufunga kwenda navyo sokoni au misibani. Haikuzoeleka sana kuwa vazi ambalo mtu anaweza kuvaa kwenda nalo ofisini ama kwenye sherehe Fulani kama sio kitchen party inayomhitaji kuvaa hivyo
'Binafsi nalipenda / Nalihusudu Vazi la kitengo' ni maneno ya Mwanadada Devotha David maarufu kama 'Devotha Jeans'pichani kuhoto akiwasha kiberiti nakusema;'Mpo on fire'!!
  Katika kubaini na kutambua nini kinaendelea nagundua wadau hawa wamekutana na kufurahi kwa pamoja ikiwa ni sehemu ya utaratibu wao mara kwa mara.
 Kulia ni Mdau Jess Jane(Jesca)hii ni furaha ya kuwa na kitu kizuri au ya kutazamia kitu kizuri.
Kutoka  Kushoto ni mwanadada Aneth (mtaalam wa maswala ya Saloon)
 Neema Kish Kish maarufu kama(Sweet-Akeel) na Bibi Lorraine Nancy Mollen
Bi Devotha David na Kijana .Hasheem Omary Said ,yeye upenda kuitwa' Omwami Hashim
 Wachezaji wa Pool Table wakiendelea kuonyeshana uwezo.
 Sehemu ya Wachezaji wa Coffee Tree Pool Klab
 Mh. Matete akifuatilia mchezo wa Pool kwa karibu.
Katikati ni Mdau Rackson Kahabuka katika hali ya utulivu, kulia ni Mdau Eugen Kabendera
Nashindwa kuelezea mfano wa kitu kinachopendwa, chenye kupendeza hivi ndivyo ilivyo kila siku katika kiwanja hiki cha New Coffee Tree Hotel. 
 Sehemu ya Wahudumu wa New Coffee Tree Hotel
 Mbele ya Camera yetu pasipo zengwe, kokoro wala Stress ndivyo anavyo onekana 'Omwami' Kijana Hasheem katika picha na mmoja wa Staff wa New Coffee Tree Hotel,Hakika Umependeza Kijana Credit kubwa kutoka Bukobawadau Blog tunakumbukumba hivi karibuni mwanamitindo wetu wa hapa Tanzania ajulikanaye kama Hassanal amefanya vizuri sana kwa mavazi ya kiafrika katika maonyesho ya mavazi ya kiafrika yaliyofanyika Afrika Kusini. Hii inaonyesha jinsi vazi la kitenge lilivyopanda chati na linavyozidi kupanda chati kwa kasi sana kwa Tanzania na kwa nchi nyinginezo za Afrika.
Kwetu sisi wanamtandano kunakitu kinaitwa TRN  hii ni katika 'Tracking' kugundua nini kinacho na kilichojili
 Mwanalibeneke anakuangazia Viwanja vya Gymkhana, Bukoba Club kuona nini kinacho endelea jioni hii.
Ndizi Choma Na Nyama Choma mezani.
Uso kwa uso na Wadau kutoka pande za Arusha na wengine wa Mjini ikiwa wamefika hapa kupata chakula cha usiku .
 Wadau wakitafakali jambo huku wakiubiri Msosi
Kushoni ni Uncle Kaitaba akipata mulo na kubadilihana mawazo na Mdau Abdul Goronga.

 Katikati anaonekana Mdau Rutta.
 Mdau Avevan wa Tiba akiteta jambo na Mdau Cathbert Basibila.
 Pamoja na yote yaliyojili, hii ni furaha kidogo mbele ya Camera ya Bukobawadau
 Mdau Samwel kuhoto,Mama Kitobo na Mr Ave wakiendelea kupata mulo.
 Anaingia katika eneo hili Mdau Bube.
Wadau wakiendelea kupata kitu menu.




 

Next Post Previous Post
Bukobawadau