KAMACHUMU YAPENDEKEZWA WILAYA MPYA
MKUU wa Wilaya (DC) ya Muleba, mkoani Kagera, Lembris Kipuyo
MADIWANI wa halmashauri ya wilaya ya Muleba mkoani
Kagera jana wameazimia kuigawanya wilaya hiyo kuwa wilaya mbili ili kurahisisha
upatikanaji wa maendeleo ya wananchi ili kujipatia huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na utawala
wa karibu kwa baadhi ya kata za mbali na Muleba.
Katibu wa madiwani wa Chama Cha Mapinduzi wilayani
humo Fortunatus Wazia amesema wilaya hiyo kijografia ni kubwa kwa kuwa na kata
43 na vijiji zaidi ya 160 ambapo upatikanaji wa huduma za jamii huchelewa.
Wazia amesema
katika kuigawa wilaya hiyo kamati ya madiwani wa CCM inapendekeza ramani
iliyochorwa kugawa wilaya hiyo katika
majimbo ya uchaguzi mipaka hiyo itumike
kwa wilaya mpya inayopendekezwa.
Aidha alisema kuwa kisiwa cha Goziba ambacho kiko
mpakani mwa mkoa wa kagera na mwanza kikimilikiwa na wilaya ya Muleba kiendelee
kuwa mkoani kagera badala ya kupelekwa wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza.
Kauli hiyo imeungwa mkono na kambi ya upinzani chini
ya msemaji wake diwani wa kata ya Kishanda
Alfred Pastory (CUF) ambaye alisema kwa kuzingatia maoni ya wataalamu na
jografia ya wilaya makao makuu ya wilaya mpya pawe kata ya Izigo.
Alitaja sababu za kupendekeza kata hiyo kuwa makao makuu ya wilaya kuwa ni kuwepo maeneo mapana ya kujenga ofisi na miundombinu nyingine kuliko kupeleka makao makuu kata ya Kamachumu panapohitaji kutoa fidia ya ardhi
Alitaja sababu za kupendekeza kata hiyo kuwa makao makuu ya wilaya kuwa ni kuwepo maeneo mapana ya kujenga ofisi na miundombinu nyingine kuliko kupeleka makao makuu kata ya Kamachumu panapohitaji kutoa fidia ya ardhi
Pichani ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya
wilaya Muleba Alhaji Swaibu
Pamoja na maoni hayo baadhi ya madiwani walivutana
katika kupendekeza makao makuu ya wilaya diwani wa kata ya Kashasha Jonathan Manwah
alipendekeza Kamachumu iwe jina la wilaya mpya na makao makuu kwa kuzingati
maoni ya wataalamu pawe izigo kauli iliyoungwa mkono na madiwani walio wengi
Hata hivyo Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya
wilaya hiyo Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya
wilaya hiyo Alhaji Swaibu Mfuruki na Mkuu wa wilaya ya Muleba Lambris Kipuyo waliwataka madiwani hao kuhakikisha
wanashirikiana na wananchi pamoja na serikali kuhimiza a maendeleo hasa
upatikanaji wa huduma za jamii
MULEBA: Na Shaaban Ndyamukama
MULEBA: Na Shaaban Ndyamukama