MATUKIO YA MWENGE WILAYANI NGARA
Mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu akikiri kupokea mwenge wa uhuru kutoka
kwa mkuu wa wilaya ya Karagwe Dary Rwegasira
katika kijiji cha kasulo wilayani Ngara.
Dc ngara akipokea mwenge kutoka kwa DC wa karagwe Mkuu wa wilaya ya Karagwe Dary Rwegasira akikabidhi mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu katika kijiji cha kasulo wilayani Ngara
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mt.Alfred Rulenge wilayaniu Ngara wakigusa
na kupokea mwenge wa uhuru ulipotembelea shule hiyo kuzindua shambala miti
12mil katika mashamba matatu ya shule hiyo
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mt.Alfred Rulenge wilayaniu Ngara wakigusa
na kupokea mwenge wa uhuru
Mwenge umekabidhiwa kutoka wilayani Karagwe na mkuu wa wilaya hiyoa
Dary Rwegasira aliukabidhi kwa mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine
Kanyasu eneo la Benako kata ya Kasulu wilayani Ngara majira ya saa
2asubuhi ya leoMara baada ya kuupokea Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Kanyasu alisema ukiwa wilayani kwake utazindua kukagua kfungua na kuweka mawe ya msingi miradi saba yenye thamani ya shilingi Bil 1 na milioni 213
Alisema
miradi hiyo ni katika sekta ya maji eneo la Benaco kilimo kwenye shamba
la migomba la Samweli Kapalala, Kuzindua Kibanio cha Mifugo Nyakisasa
(Tsh 12mil) na
kuweka jiwe la msingi Kituo cha Afya kijiji cha Kashinga kata ya
Nyakisasa
Aidha
alisema mradi mwingine ni hifadhi ya mazingira katika shule ya
sekondari Rulenge ambayo imepanda miti 12mil na malengo ni kufikisha
miti 30mil ambapo kila manafunzi hupanda miti 5 kwa kila mwaka
Pamoja
na hayo mwenge huo umezindua jengo la utawala katika Shule ya sekondari
ya Rhec English Medium kata ya Rulenge na hatimaye kutoa cheki ya
mikopo sacos ya vijana mjini Ngara
Mkesha
wa mwenge umefanyika katika viwanja vya posta ya zamani mjini Ngara na
utakabidhiwa kwa mkuu wa wilaya ya Biharamulo Richard Mbeo katika kijiji
cha Nyabugombe kata ya Nyakahura .