MATUMIZI YA MITANDAO NA ATHARI ZAKE
Tuongelee matumizi ya mitandao na athari zake!
Jamani sisi wana wa kizazi hiki tumekuwa digitalized mno,kila mtu anachofanya kwenye maisha yake kipo kwenye mitandao tofauti ya jamii kama ni facebook,twitter,instagram n.k Wenzangu mnalichukuliaje swala hili?
NAKAA NIKIJIULIZA TUNAPOTEZA SIFA ZA KUSOCIALIZE KIKAWAIDA MPAKA TUMEKUWA WATUMWA WA MITANDAO TOFAUTI
Hata mtu akila apple ata andika na picha atajipiga akilitafuna
Imekuwa kama fasheni kwa sasa kuweka picha zisizo na maadili pamoja na kuwa na marafiki wengi tusiowafahamu walio katika mabara tofauti ya dunia.Je athari za kuweka picha zetu na personal information kwenye mitandao tofauti tunazipa uzito gani?
Kwa wazazi athari za kuweka picha za watoto wetu ambazo tunajua wakija kukua zitawaaibisha na hata kuwaathiri tunalichukuliaje?
Nakubali kuna faida nyingi za mitandao hii na imeunganisha watu wengi,lakini je tunaitumia ipasavyo?Kama sasa hali ipo hivi miaka 10 ijayo itakuwaje?sidhani kama hata watu wanasemeshana kwa midomo,kila aina ya mawasiliano itakuwa kwa maandishi,kupitia kwenye simu,computer n.k
Athari zake kiafya lipoje?madaktari mnakaribishwa kuliongelea hili,nchini china asilimia kubwa ya watoto wanavaa miwani kutokana na muongezeko wa kutumia vifaa vya kidijitali!Je tunawalemaza watoto na uwezo wao wakujichanganya na watoto wengine kwa matumizi ya vifaa tofauti vya kiteknolojia?Je tunawapunguzia uwezo wao wa kuwa kuunda michezo ya aina tofauti kwa hali hio?
Je mitandao hii inajenga au inabomoa?