MWANAFUNZI AUAWA NA KUNYOFOLEWA VIUNGO VYA MWILI
MULEBA:Na Shaaban Ndyamukama May 2014
Mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya
msingi Kitunga wilayani Muleba mkoani Kagera ameuawa na mganga wa kienyeji kwa
kunyonga kisha kumzika nyumbani kwake kwa kile kilichodaiwa ni imani za
ushirikina
Afisa mtendaji wa kata Muhutwe wilayani Muleba Wilson Charles
amesema mwanafunzi huyo wa kike (8) jina limehifadhiwa (Furaha Jofule) aliuawa
juzi katika kijiji cha Bisole kwa
kukatwa viungo vya mwili kisha kuzikwa kichwa chini miguu juu
Bw Charles amesema kuwa walikuwa wananfunzi wanne
wakielekea shuleni na walipofika njiani waliitwa na mganga wa kienyeji Juma
Busigwa ambapo watatu walikataa na
kukubali mmoja wao na ndipo alimkamata kisha kunyonga
Amesema katika kufanya kitendo hicho kwanza alimkata
sehemu zake za siri masikio sehemu ya mabega na kukata mkono wa kushoto ambapo
alichimba chimo katikati ya mafiga na kutunza viungo hivyo vya mwili wa mtoto huyo
“Alipomaliza kuficha viungo ndani ya nyumba
alichimba tena shimo kubwa na kumwinamisha kwa kutanguliza kichwa kisha kiuno
na miguu kubaki nje yaani alifukia nusu ya kiwiliwili” Alisema Charles
Aidha amesema taarifa za mwanafunzi huyo kuuawa
zilipatikana baada ya kutafutwa shuleni bila kupatikana hadi kesho yake ambapo
wenake aliokuwa nao ndio walitaja mazingira alipopotelea na alipatikana kwa
mganga huyo saa7 mchana
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Bisole Philbert Ludovick amesema hilo ni tukio la
pili katika kijiji hicho kwani mwaka juzi mwanafunzi wa kike alipotea katika
mazingira ya kutatanisha na kupatikana akiwa amechunwa ngozi
Alisema vitendo vya mauaji na kuchukua viungo vya
mwili vinafanywa na wageni kutoka nje ya mkoa wa kagera wanaotafuta kupata
utajiri wakijiingiza kwenye biashara mbalimbali kwenye maeneo yanayokua
kiuchumi na kimaendeleo
“Tuna mji wa Izigo na Kaboya wanakuja watu wengi
kuendesha maisha yao lakini licha ya kuwasajili kwenye madaftari ya vitongoji
wanaishi kwa kuhama hama na kusabaisha wasitambulike shughuli zao kwa undani”.Alisema
Ludovick
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Bw George Mayunga amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa ambaye amekiri kufanya mauaji hayo
anashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano zaidi