SKYLIGHT BAND WALETA HOMA YA BURUDANI NDANI YA JIJI LA DAR, NJOO UTIBIWE THAI VILLAGE IJUMAA HII KWA BURUDANI YA NGUVU
Sam Mapenzi akiamsha amsha Taratibuuuuuuu ndani ya Thai Village.
Winfrida Richard akiimba kwa sauti nyororooooo kabisaaaa amsha amsha kwa mashabiki ndani ya Thai Village Ijumaa iliyopita.
Sam Mapenzi kushoto akiwa na Winfrida Richard wakitoa vocal za ukweli kuwapa raha mashabiki wao ndani ya Thai Village.
Aneth Kushaba AK47 toka kulia akiongoza makamuzi ndani ya Thai Village Ijumaa iliyopita.
Joniko Flower kushoto akiongoza makamuzi ya sebene kaliii akipewa sapoti na Sony Masamba.
Hapo sasa Mzuka umeanza kupanda mpaka Sony Masamba kapandisha suruali juu chezea sebene wewe.
Daudi Tumba akizipiga Tumba kwa ufasahaa mkubwa kabisaaa kutoa burudani kali ndani ya Thai Village Ijumaa iliyopita.
Mpiga kinanda mahiri wa Skylight Band AMOS KINANDA akicharaza vizuriiii vitufe vya kinanda hicho kutoa burudani kaliiii ndani ya Thai Village Ijumaa iliyopita kwa mbali mpiga drums mahiri Idrisa akiwajibika.
Hashim Donode mwenye tisheti nyeusi akizitoa vocal kali akipewa sapoti na Aneth Kushaba pamoja na Digna Mbepera.
Hahahaha weweeeee umeona stepu izo za Aneth Kushaba AK 47 na Hashim Donode mwenye Tisheti nyeusi hapo ni kuwapa raha mashabiki wao ndani ya Thai Village.
Digna Mbepera mwenye Top ya njano akifuatiwa na Aneth Kushaba pamoja na Hashim Donode wakiwa na furaha teleeee huku wakiyarudi mauno kuwapa burudani mashabiki wao ndani ya Thai Village.
Kibegaaaa Kibegaaa hapo ni Aneth Kushaba na Hashim Donode wakiwachezesha mashabiki wao ndani ya Thai Village.
Raha kweli kweli hao ni mashabiki wa Skylight Band Dimo Debwe na Sillas Mbuya wakiwa na mdau wao wakipata Ukodak wa nguvu.
Ukodak time hapo Ni Aneth kushaba wa kwanza kulia,Winfrida Richard na Digna Mbepera wakifurahia miale ya kamera.
Sam Mapenzi akitoa bass vocal ya nguvuuu ndani ya Thai village Ijumaa iliyopita.
Sam Mapenzi akiweka swagga na manjonjo kunogesha mziki kwa mashabiki wa Skylight Band.
Joniko Flower baba ya Congo akiimbisha vilivyo na vocal zake kali.
Kikuku uyooooo ana manyoyaaa uyoooo Kwiooo Kwiooooo staili tamu na inayo wakuna mashabiki wa Skylight ikichezwa vilivyo na Aneth Kushaba na Sam Mapenzi njooo Ijumaa hii ujifunze kucheza.
Chezea watoto wa mjini wewe unaona mastaili hayo makali ya vijana wa Skylight Band.
Hapo sasa Aneth Kushaba akiongoza vijana wake kutoa burudani kaliiii ndani ya Thai Village.
Joniko Flower akionyesha kwamba na yeye anaweza kuyarudi.
Hapo sasa Jonikoooooo kiuno feni....!
Wadau wa Skylight Band toka Kushoto Nkina, Dada Josephine na Mdau.
Aneth Kushaba aliamua kushuka stejini na kuamua kuyarudi akiwa chini baada ya kupagawa na mziki mzuriiii toka kwa vijana wake.
Hahaha Hapo ni mduaraaa unaanza taratibuuuu.
Zungushaa zungushaaa mashabiki wakijipanga kuucheza mduara.
Kaka hapo kati akiusakata mduara kwa raha zake na dada kwa mbaliiii akizungusha nyonga.
Haya sasa kama una nyonga kweli shika kiti tuone kiuno chako lainiiii.
Mikono juuu Mikono juuuu kama una furaha hapo ni mashabiki wa Skylight wakichezeshwa kwa Raha zaoooo.
Mashabiki wakichizika.
Safiii dada akiburudikaa na mziki mzuri toka kwa Skylight.
Nyomiii la kutoshaaa ndani ya Thai Village Ijumaa iliyopita tukutane leo pia kwa burudani zaidi.