TASWIRA NA CHANGAMOTO ZA WATUMISHI WILAYANI KARAGWE
Wilaya ya Karagwe inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa watumishi kuanzia
ngazi za vijiji hadi wilaya hali inayopelekea kukwamisha shughuli za utoaji
huduma kwa wananchi.
Mtaa kwa mtaa Camera yetu inakutana na Rasta mmoja maarufu Wilayani Karagwe
Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe imedhamiria kuwa, katika kipindi cha miaka tisa ijayo, wananchi wa Wilaya hii kwa jinsia zote walioko Wilaya hii wawe jamii yenye maisha bora, inayowajibika kwa maendeleo yake, uchumi imara na endelevu na uongozi unaozingatia mipango shirikishi na utawala wa kisheria ifikapo 2025
Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya
Karagwe Dary Ibrahimu Rwegasira katika
kikao cha Baraza la madiwani
kilichofanyika juzi kwenye ukumbi
wa kituo rafiki cha Vijana maarufu kama
angaza kilichopo mjini Kayanga wilayani
hapa.
Jengo la Halmashauri ya Wilaya Karagwe.Mtaa kwa mtaa Camera yetu inakutana na Rasta mmoja maarufu Wilayani Karagwe
Alisema kuwa wilaya inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo
upungufu wa watumishi kuanzia ngazi ya vijiji,kata na wilaya hali inayosababisha kukwamisha utoaji huduma
kwa uhakika na kuchelewesha maendeleo kwa wananchi.
Rwegasira alisema kuwa changamoto nyingine zinazoikabili wilaya ya
karagwe ni ugonjwa wa mnyauko wa migomba
na ukame ambazo zimeathiri sana maendeleo ya wilaya kwani wananchi
na wenyeji wa Karagwe hutegemea kilimo cha migomba na mazao mbalimbali
ya chakula hivyo ukame umeathiri sana
shughuli za kilimo.
Aidha,alibainisha kuwa vitendo vya
unyanyasaji wa kijinsia na ubakaji
kwa mwaka 2013 vimeongezeka tofauti
na miaka mingine ni kutokana na
kutokuwepo ushirikiano wa wahusika na vyombo vya dola.Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe imedhamiria kuwa, katika kipindi cha miaka tisa ijayo, wananchi wa Wilaya hii kwa jinsia zote walioko Wilaya hii wawe jamii yenye maisha bora, inayowajibika kwa maendeleo yake, uchumi imara na endelevu na uongozi unaozingatia mipango shirikishi na utawala wa kisheria ifikapo 2025