WADAU WA BANDARI NA RELI WA TANZANIA WAKUTANA NA TAASISI YA UWEKEZAJI KATIKA NCHI ZINAZOENDELEA YA UBELGIJI
Wadau wa Bandari na Reli wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na
Uongozi wa Taasisi ya Uwekezaji katika nchi zinazoendelea ya Ubelgiji
(BIO)baada ya kumaliza kikao cha kuishawishi taasisi hiyo kuwekeza
katika miradi mbalimbali ya kukuza uchumi na kupambana na umaskini
Tanzania. Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala
(mwenye tai yenye rangi za bendera ya taifa) ameongoza ujumbe huo.
Aidha, Balozi Kamala amemuomba Bwana. Luik Zonneveld Mkurugenzi Mkuu wa
taasisi hiyo (kushoto kwa Balozi Kamala) kushirikiana na Tanzania
kutafuta fedha za kuwekeza katika miradi mikubwa ya reli na bandari
Tanzania. Mkurugenzi huyo amekubali ombi la Balozi Kamala.