WAKIMBIZA MWENGE WAZAWADIWA MIKUNGU YA NDIZI -NGARA
Kaimu kiongozi wa
mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa Hamza Muhamudi akikata mkungu wa ndizi katika
shamba la migomba la Samweli Kapalala (Kulia kwake) katika kijiji cha
Kasulo Wilayani Ngara mkoani Kagera baada ya kupewa kama zawadi
Watanzania wametakiwa kutumia ardhi kama rasilimali ya kujikwamua kiuchumi kwa kufanya kazi kwa bidii na kunufaika na matunda yanayopatika baada ya kuzalisha mali kupitia miradi ya kilimo na mifugo kujipatia maendeleo
Muhamud amesema licha ya wakulima wa migomba mkoani kagera kushambuliwa na ugonjwa wa unyanjano na kukosa chakula kwa kutumia utaalamu wa kisasa na kilimo bora ugonjwa huo unaweza kutokomea haraka
Amesema kitendo cha mkulima kutumia mtaji wake wa ardhi na mifugo kidogo kuandaa shamba na kutoa mazao yenye soko katika wilaya nzima na mkoa ni jambo la kuigwa katika uchu wa kujiletea maendeleo ya familia wilaya na mkoa
NGARA: Na Shaaban Ndyamukama
Watanzania wametakiwa kutumia ardhi kama rasilimali ya kujikwamua kiuchumi kwa kufanya kazi kwa bidii na kunufaika na matunda yanayopatika baada ya kuzalisha mali kupitia miradi ya kilimo na mifugo kujipatia maendeleo
Kaimu
kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru
Kitaifa Hamza Mohamudi ametoa wito huo jana wakati akikagua shamba la mkulima
wa zao la ndizi katika kijiji cha Kasulo wilayani Ngara mkoani kagera
Kaimu
kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru
Kitaifa Hamza Mohamudi ametoa wito huo jana wakati akikagua shamba la mkulima
wa zao la ndizi katika kijiji cha Kasulo wilayani Ngara mkoani kagera Muhamud amesema licha ya wakulima wa migomba mkoani kagera kushambuliwa na ugonjwa wa unyanjano na kukosa chakula kwa kutumia utaalamu wa kisasa na kilimo bora ugonjwa huo unaweza kutokomea haraka
Amesema kitendo cha mkulima kutumia mtaji wake wa ardhi na mifugo kidogo kuandaa shamba na kutoa mazao yenye soko katika wilaya nzima na mkoa ni jambo la kuigwa katika uchu wa kujiletea maendeleo ya familia wilaya na mkoa
Aidha
amempongeza mkulima wa migomba Samweli Kapalala ambaye shamba lake alilianzisha
mwaka 2003 kwa kianzio cha ekari mbili
ambapo sasa limefikia ekari 6.5 likiwa na miche au mashina 444 ya
migomba.
“Ndugu yangu
sinabudi kukushukuru kwa jitihada na nguvu kazi unayotumia katika shamba hili
na vijana uwarithishe kwa kuwaelekeza mbinu na mtaji ulioanza nao ili
waondokane na umaskini”.Alisema Mohamudi
Akitoa
taarifa za mradi wa shamba hilo Samweli Kapalala alisema katika shamba hilo hupanda migomba inayotoa ndizi aina ya Nchakala na sehemu ya shamba amepanda migomba aina ya
FIA 17& 23 kwa kutumia wataalamu wa kilimo
Alisema mkungu
wa ndizi unauzwa kati ya Sh 15,000/-kwa aina ya Nchakala na Sh 35,000/ kwa
ndizi aina ya FIA 17& 23 ambapo katika faida aliyokwisha pata ni kusomesha
watoto kununua ng’ombe kupata mbolea na
amejenga nyumba bora
“Natumia
shamba hili kufundishia wakulima wa ndani na nje ya nchi na shamba
hili limeniwezesha kuwa mshindi wa kwanza kimkoa mwaka 2012 na wa pili kwa
mwaka 2013 katika maonesho ya nanenane
kikanda”.Alisema Kapalala
Pamoja na
faida hiyo alisema tangu kuanzishwa kwa shamba hilo hadi sasa lina thamani ya
Sh250,000,000 lakini katika uzalishaji zimeshapatikana Sh 375 mil ingawa
changamoto ni ukosefu wa soko na ugonjwa wa unyanjano NGARA: Na Shaaban Ndyamukama