AJALI MBAYA YATOKEA ASUBUHI YA LEO ENEO LA BUNAZI,WATU WAWILI WANUSULIKA KIFO!!
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 3:00 asubuhi ya leo June 9,2014 katika Kijiji cha Kabwela Kata ya Bunazi ,Wilayani Missenyi,Watu wawili wamenusulika kufa katika ajali hiyo, watu hao ni Mfanyabiashara maarufu wa Mutukula ajulikanaye kama Mr Morgan akiwa na Afisa Uhamiajia anayejulikana kwa jina la Daudi Mwala.
Mpaka jioni hii Majeruhi wamelazwa katika hospital ya Mkoa iliyopo Mjini Bukoba
Gari aina ya Toyota Harrier yenye nambari za Uganda UAT740D lilikuwa likitokea Kyaka Mjini kuelekea Mutukula, limepoteza mwelekeo na kuacha njia kuu huku likiwa na mwendo mkali na kuelekea bondeni njia panda kuelekea kiwanda cha Sukari cha zamani Kagera A.