Madiwani hao kutoka vyama tofauti walifunguliwa kesi mahakamani na Diwani wa Kata ya Kahororo, Chifu Kalumuna (CCM) kuwa hawana sifa za kuendelea kuwa madiwani.
Kalumuna, ambaye pia ni Mwenyekiti wa UVCCM Manispaa ya Bukoba na
Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Uchumi alifungua shauri dhidi ya
madiwani hao kuwa wamepoteza sifa za kuendelea kuwa madiwani kwa
kushindwa kuhudhuria vikao vya kisheria bila taarifa.
Madiwani
walalamikiwa katika kesi hiyo walikuwa ni Diwani Yusuph Ngaiza (Kashai
CCM), Dauda Kalumuna (Ijuganyondo CCM), Samwel Ruhangisa (Kitendagulo
CCM) na Deusdedith Mutakyahwa wa Kata ya Nyanga CCM.
Wengine ni
Richard Gaspar (Miembeni CCM), Mulungi Kichwabuta (Viti Maalumu CCM),
Israel Mulaki (Kibeta CHADEMA) na Rabia Badru (Viti Maalumu CUF).
Baada ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kusoma
taarifa ya ukaguzi kwenye manispaa hiyo, madiwani walitakiwa kuanza
vikao mara moja.
Hata hivyo, Kalumuna aliweka pingamizi dhidi ya
madiwani hao kutohudhuria vikao mpaka itakaposikilizwa kesi ya msingi
aliyofungua dhidi yao.
Baada ya mahakama kupitia hoja za
mlalamikaji na walalamikiwa kupitia kwa mawakili wao, Hakimu wa mahakama
hiyo, Charles Uisso alisema mahakama hiyo ina uwezo kisheria kusikiliza
shauri lao na kutaka upande wa walalamikiwa kupeleka hoja nyingine za
msingi kama zitakuwapo.
Upande wa walalamikiwa walianza
kuwasilisha hoja mpya za utetezi Machi 3, kwa uamuzi huo vikao vya
Baraza la madiwani viliendelea kusimama kusubiri uamuzi wa mahakama.
Walalamikiwa walikuwa wanatetewa na Wakili Mathias Rweyemamu, huku mlalamikaji ukiwakilishwa na Wakili Aaron Kabunga.
Chanzo cha kesi hiyo ni mgogoro ambao umechukua muda mrefu na kusimama
kwa maendeleo kati ya Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki na
Meya wa Manispaa hiyo, Dk Anatoly Amani.
Haijulikani kama uamuzi huu wa mahakama utatuliza hali ya hewa katika manispaa ya Bukoba.

ZILIZO TAZAMWA ZAIDI
DOWNLOAD 'PANAPOFUKA MOSHI 'BY JUSTIN KALIKAWE
13 Aug, 2013
Marehemu Justin Kalikawe ndani ya 'Panafufuka MOTO' fanya kudownload na kusikiliza mashairi yake, kikubwa ni maswala ya ajira kwa ...
13 AUG, 2013 NI KUMBUKUMBU YA MIAKA 10 YA KIFO CHA MWANAMUZIKI JUSTIN KALIKAWE KILICHOTOKEA 13AUG, 2003
13 Aug, 2013
7
Kutoka maktaba ya bukobawadau blog, hivi ndivyo mazishi ya marehemu Justine Kalika yalivyokua , kijijini kwake KITENDAGURO kibeta ndani y...