Bukobawadau

BREAKING NEWS;PROF.ANNA TIBAIJUKA APATA AJALI,YU SALAMA .

Taarifa zilizoufikia mtandao ni kwamba waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Prof Anna Tibaijuka amepata ajali baada ya gari alilokuwemo kuparamia punda katika mji wa kahama,akiwa njiani kuelea mjini Dodoma.
 Akiongea kwa simu afisa habari wa waziri huyo Bw Kamanzi amesema kuwa ni kweli gari la waziri huyo limepata ajali lakini anamskukuru mungu haikusababisha madhara makubwa. 
 "Ni kweli gari la waziri limegonga Punda hapa Kahama baada ya Waziri kupitia Mkoani Geita katika shughuli za ulezi wa Mkoa huo,lakini ajali hiyo haikuwa kubwa sana,madhara yalikuwa madogo na hivi sasa tunapoongea, tunaendelea na safari kuelekea Bungeni Dodoma na kesho utamuona Waziri akijibu hoja,hivyo yuko salama" alisema Kamanzi.
Next Post Previous Post
Bukobawadau