HATI ZA VIWANJA MANISPAA BUKOBA
Marafiki wapendwa
Pamoja
na changamoto, Manispaa ya Bukoba imeandaa hati zaidi ya hati 1,000 kwa
walioomba na kulipia viwanja katika mradi wa viwanja 5000.
Orodha hii inajumuisha:
1.
Hati ambazo zimeandaliwa, hivyo kuwaomba wahusika kusaini hati hizo.
Unaweza ukatuma mwakilisha kukuchukulia ili uweze kusaini na kurejesha
ofisi za Manispaa-Idara ya Mipango Miji na Ardhi.
2.
Hati ambazo zimekamilika yaani zimeidhinishwa na Kamishina na
kusajiliwa na Msajili wa Ardhi Mwanza. Waweza kufika ofisini au kutuma
mwakilishi akiwa na Power of Attorney kuchukua hati yako. Hati nyingi
zimepelekwa Mwanza ili ziweze kuidhinishwa na kusajiliwa lakini kidogo
kutoka kwake ni kudogo sana. Tumewasihi wahusika waweze kuongeza kasi
ya kuidhinisha na kusajili.
Wale
ambao majina yao hayaonekani na tayari wamekamilisha malipo, tunawaomba
wawe na subira, tunaendelea kuandaa. Tutawajulisha kwa simu kama
ambavyo tumekuwa tukifanya.
Mjulishe jamaa, rafiki na nduguyo.
RAI:
Waliopata viwanja waanze kujenga, shukrani kwa wachache ambao tayari
wameanza pia walipe kodi ya ardhi kwa maendeleo ya Manispaa na Taifa kwa
ujumla.
Kujua hatua ya maandalizi ya hati wasiliana na Fauzia Kimaro (0754775309)
Tushabire Bukoba na Kagera
Inawezekana.