HISTORIA YA MAISHA YA MREMBO MILLEN MAGESE
HAPPYNES
MILLEN MAGESE jina hili sio adimu sana masikioni mwa watanzania walio
wengi,huyu ndiye aliyewahi kuwa miss Tanzania mwaka 2001 na kujizolea
umaarufu wake hapa nchini na nje ya Tanzania.
Pamoja na kuwa miss Tanzania mrembo huyu amebahatika kuwa na kipaji
cha uwana mitindo kipaji ambacho kimempa mafanikio makubwa hata kumpa
umaarufu wa dunia kwa shughuli hiyo ya uwanamitindo.
Mrembo huyu baada ya kufanikiwa kuwa miss Tanzania alifanikiwa
kuhamia nchini Africa ya kusini ambako alianza kufanya kazi zake za
uwana mitindo na kujizolea umaarufu mkubwa sana na baadae kuishi pia
nchini marekani kwa ajili ya kazi hiyo hiyo
Historia ya binti huyu ni kubwa sana kwani ni moja kati ya warembo
wa Tanzania waliotumia vizuri nafasi walizopata kwa ajili ya
kujiendeleza na kupata mafanikio
Kabla
ya MILLEN kuwa miss Tanzania akiwa na umri wa miaka 15 tu alianza
kupata tatizo ambalo lilikuwa linamkosesha raha sana tatizo ambalo kwa
hapa Tanzania walishindwa kujua nini kinamsumbua hasa,kwani alikuwa
akipata maumivu makali wakati wa hedhi kwa wale wanawake wanaelewa,na
pia alikuwa hana muda ama kipindi maalum cha kuingia katika hedhi muda
wowote alikuwa anaweza kuingia na kupata maumivu makali sana.
Baadhi ya
wanafunzi ambao pia wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo hilo wakiwa katika
semina hiyo iliyoandaliwa na mrembo MILLEN MAGESE wikiend hii jijini dar
es salaam
MILLEN MAGESE anapokumbuka mateso aliyopitia haachi kulia hata mbele za watu kwa inauma sana,katika semina hii alimwaga chozi
Tatizo
hilo lilimsumbua kwa takribani miaka yote ambayo aliyokuwa nchini na
madaktari nchini walishindwa kujua nini hasa kunamsumbua.MILLEN baada ya
kwenda kuishi Africa ya kusini tatizo hilo lilizidi sana na kuamua
kuwaona wataalam mbalimbali nchini humo kwa ajili ya vipimo ambapo walifanikiwa kujua ni tatizo gani lilimpata.
ENDOMETRIOSISI ni ugonjwa ambapo ni mgeni sana masikioni mwa
watanzania ambapo hata kishwahili chake bado hakijapatikana ni ugonjwa
ambao humsababishia mgonjwa maumivu makali sana kipindi cha hedhi na
husababisha pia mgonjwa kutopata mtoto.
Huu ndio ugonjwa uliomkuta mrembo MILLEN MAGESE ambapo ilibidi
afanyiwe upasuaji wa kizazi kwa mara 12 nchini Africa ya kusini kwa
ajili ya kutibu ugonjwa huo jambo ambalo linasikitisha sana.
akitoa semina
“Nimefanyiwa
upasuaji wa kizazi mara 12 nchini Africa ya kusini kwa msaada wa
marafiki zangu ili kuokoa maisha yangu,sina uwezo wa kupata mtoto tena
mirija yangu yote imeziba na madactari wanasema haiwezi kuzibuka
tena”aliiambia habari24.
Mrembo huyo kwa sasa yupo nchini na HABARI24 BLOG imefanikiwa kukutana
naye na kufanya naye mahojiano maalum ambapo ametueleza lengo lake la
kurudi nchini Tanzania
“Nimekuja
Tanzania sasa kwa lengo moja kuwaokoa watanzania na kuwajengea uelewa
juu ya ugonjwa huu chini ya mpango wangu wa MILLEN MAGESE FOUNDATION
,kwa sababau ugonjwa huu kwa hapa Tanzania unaonekana bado haufahamiki
japo watu wengi sana unawasumbua kiasi kwamba wanakosa raha maishani na
kikubwa zaidi hakuna hata kipimo cha ugonjwa huo hapa nchini
Tanzania”aliiambia HABARI24 BLOG
Kwa kuanza na hilo la kuwaelimisha watanzania wikiend hii mtandao huu ulimshughudia mrembo MILLEN akiwa anatoa semina kwa wanafunzi,kina mama na watanzania zaidi ya mia moja juu ya ugonjwa huu ambapo walimshukuru sana kwa huduma hii.
Katika maongezi yake MILLEN ameigeukia serikali na kuiomba kuhakikisha
unawasaidia wagonjwa wa ENDOMETRIOSIS ikiwa ni pamoja na kuwajengea
hospitali maalum ya ugonjwa huo
USIKOSE HAPA HAPA TUTAKUPA USIKIE SAUTI YAKE AKIZUNGUMZA NASI