MARADONA AWABWATUKIA FIFA KWA KUIKOSEA HESHIMA COSTA RICA.
Nguli wa soka duniani na mkali wa enzi hizo wa Argentina, Diego
Armando Maradona, amewafananisha viongozi wa FIFA na genge fulani la
wahuni lisilo na nidhamu wala heshima,
kufuatia hatua ya shirikisho hilo la vyama vya soka duniani, kuamuru
kuchukuliwa mkojo kwa wachezaji saba wa timu ya taifa ya Costa Rica,
waliokuwa uwanjani siku timu hiyo ilipoibamiza Italia kwa bao 1-0 na
kufuzu kwa hatua ya 16 bora.
Maradona, anaamini kuwa kitendo cha FIFA kutaka kupima mkojo wa
wachezaji hao kuwa walitumia dawa za kuongeza nguvu au laa, ni cha
kudharau mabadiliko chanya makubwa ambayo Costa Rica wameyafanya katika
mfumo wao wa soka, mabadiliko ambayo ndio yamewapa mafanikio waliyofikia
hadi sasa katika Kombe la Dunia.
VIA Jukwaa Huru Media
VIA Jukwaa Huru Media