MATUKIO MBALIMBALI MH. MBOWE AKIWA ZIARANI
Mmoja wa Wanakamati wa Kamati ya Mfuko wa Maendeleo (CDF)
Jimbo la Hai akipanga kuni katika moja ya madarasa ya Shule ya Msingi
Shirimatunda iliyoko wilayani Hai, wakati Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Freeman Mbowe (Mbunge wa Hai), alipofanya ziara ya kukagua miradi
mbalimbali ya maendeleo jimboni humo ambayo mfuko huo utasaidia kuongeza
nguvu za ujenzi.
Chumba hicho mbali ya kutumika na wanafunzi kwa ajili ya kusomea, pia kinatumika kama stoo ya kuni za kupikia chakula cha wanafunzi shuleni hapo, hali ambayo inadhihirisha kuwepo kwa mahitaji ya vyumba kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe akichungulia tundu
Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe akiwa pamoja na Kamati ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo (CDF), wakikagua Dara la Marire, Iwala, ikiwa ni sehemu ya ziara anayofanya kwa ajili ya kufanya tathmini ya miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo ambayo inahitaji kupata msukumo wa kuongezewa nguvu za ujenzi na mfuko huo ambao yeye ni mwenyekiti wake.