Bukobawadau

MDAU ABDULRASUL BWANIKA ANUSURIKA KATIKA AJALI ENEO LA RUHANGA KAMACHUMU

Mdau Abdulrasul Bwanika pichani kapata ajali mbaya ya gari iliyotokea mchana wa leo June 22, 2014 eneo la Ruhanga,barabara kuu iendayo Kamachumu kilometa chache kutoka Kijiji cha Muhutwe Wilayani Muleba.
 Baada ya tukio walikimbizwa katika hospitali ya Ndolage kwa matibabu na uchunguzi zaidi.
Ndani ya Gari hilo walikuwepo JAMAA ZAKE wawili na Sheikh aliye julikana kwa jina la Idrisa ambaye naye amejeruhiwa na mmoja wa Jamaa zake amejeruhiwa vibaya na wote wamekimbizwa Katika Hospital ya Ndolage Kamachumu.

 Katika picha ni muonekano wa Gari walilokua wakisafiria lilivyoaribika.
 Eneo lilipogonga gari baada ya kuama njia.
 Mdau Abdulrasul  na mwenzake walikua njiani kuelekea  Mjini Kamachumu katika SHUGHULI ya HARUSI ya Mdogo wake iliyofanyika Mchana wa Leo
Mdau Abdulrasul  ambaye baada ya ajali alipelekwa kwenye Hospitali ya Ndolage iliyopo karibu na eneo la tukio,amepata Jeraha la taya na maumivu makubwa kifuani ambapo alipigwa na usikani baada ya ajali hiyo kama inavyo onekana katika picha.
 Mdau Abdulrasul  na mwenzake walikua njiani kuelekea  Mjini Kamachumu katika SHUGHULI ya HARUSI ya Mdogo wake Najim Jaafar Bwanika (pichani kulia)iliyofanyika Mchana wa Leo .
Mdau Abdulrasul Kapewa dawa za maalum za kupunguza maumivu kutokana na hali yake ili afike kusalimia wageni waliohudhuria harusi ya mdogo kisha karudishwa  hospitalini kuendelea na matibabu.
Muonekano wa barabara Ruhanga maeneo ilipotokea ajali hiyo.
Mdau Yusuph Wastara eneo ilipotokea ajali iliyo husisha Gari lenye nambari T386ADS
Ndugu Abdulrasul ni Kaka Mkubwa wa Mdau Kandanda pichani kushoto
Inshallah  Mwenyezi Mungu awawekee wepesi wa kupata nafuu haraka.
Next Post Previous Post
Bukobawadau