TOFAUTI YA MUDA WA FAMILIA NA MUDA WA MPENZI WAKO
Kuna
tofauti kubwa kati ya kuwa na muda na mpenzi wako "quality time with your love" na kuwa na muda na familia "quality time with your family".
Wanaume wengi huwa wanadhani wakishakuwa na muda na familia zao ndo wamemaliza,
wanafikiri kwa kule kukaa hotelini na familia nzima mke naye tayari kashapata muda
wake na kiu yake imekata, kumbe kwa mwanamke ule ulikuwa muda wa wewe na yeye
na watoto kwa pamoja, bado muda wa wewe kuwa na yeye peke yenu. Yako mambo
ambayo kama wanandoa hamuwezi kuyazungumza mkiwa na watoto bali mkiwa peke yenu
tu, na mara nyingine hata kama hamna la kuzungumza bado mnahitaji muda wa kuwa
peke yenu. Kamwe muda wako mume na familia yako hauwezi kumridhisha mkeo kama
ambavyo mngepata muda na yeye peke yake. Wives
needs quality time with their husbands independently from the children,
husbands’ dont hide in the shadow of the kids – Chris Mauki