WAZIRI KAMANI AWAASA WANANCHI WA KAGERA KUTUMIA FURSA NZURI ZILIZOPO KUFUGA KISASA ILI KUINUA UCHUMI WA NCHI
Waziri Dk. Kamani Akipata Maelezo Jinsi ya Kuandaa na Kukausha Mabaki ya Samaki (Mapanki) Kutoka kwa Mama Kalega Mmiliki wa Kiwanda cha Mapanki Kilichopo Kemondo Lwagati
Shehena ya Mabaki ya Samaki (Mapanki) yaliyokaushwa Tayari kwa Kusafirishwa Kwenda sokoni
Mwekezaji Bw. David James Akitoa Maelezo Mbele ya Waziri Kamani Jinsi Alivyojipanga Kuwekeza Katika Sekta ya Mifugo Hasa Ng'ombe na Kujenga Kiwanda cha Kuchinja na Kusindika Nyama Katika Ranchi ya Mabale Wilayani Missenyi
Waziri Kamani Akiongea na Wananchi Eneo la Kihanga Wilayani Karagwe
Waziri Dk. Titus Kamani Akiwa Katika Picha ya Pamoja na Wanafunzi wa Chuo cha Mifugo kilichofunguliwa Hivi Karibuni Kikulula Wilayani Karagwe
Hawa ni Ng'ombe wa Mwaka Mmoja na Nusu Ambapo Wananchi Wameshauriwa kufuga Namna Hii na kuachana na Makundi Makubwa ya Ng'ombe yanayoleta Migogoro Kwenye jamii
Waziri Kamani Akikagua Kiwanda cha Kusindika minofu ya Samaki Kagera Fish Kemondo.
Waziri Dk. Kamani Akiangalia Samaki Aina ya Kambale Wanaofugwa Kwenye Mabwawa Katika Eneo la Ruhanga Wilayani Muleba
Waziri Kamani Akikagua Mabwawa ya Samaki Ruhanga Wilayani Muleba.
Wananchi wa mkoa wa Kagera wameaswa kutumia fursa ya hali ya hewa nzuri, ardhi nzuri na upatikanaji wa maji kwa wingi katika sehemu mbalimabali za mkoa kuanzisha ufugaji wa kisasa wa mifugo hasa ng’ombe na samaki katika mabwawa ili kuinua hali ya uchumi wa wananchi.
Ushauri huo ulitolewa na Waziri
wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Titus Mlengeya Kamani alipofanya ziara
mkoani Kagera kuanzia tarehe 9-11/06/2014. Mhe. Kamani alitoa wito kwa Idara na
kitengo cha doria mkoani Kagera kuimarisha doria na kuzuia uvuvi haramu.
Mhe. Kamani alisistiza viongozi
wa idara hiyo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ufugaji wa samaki katika mabwawa
ili kutoa fursa ya samaki katika ziwa Victoria kuzaliana zaidi. Ushauri huo
aliutoa alipotembelea ofisi za uvuvi katika Manispaa ya Bukoba eneo la Custom Karibu na bandari ya Bukoba.
Pia Mhe. Kamani alihaidi kuwa
serikali itaendelea kutoa ushirikiano na msaada wa kitaalam kwa wawekezaji ambao
wanajishughulisha katika sekta za viwanada vya kuchakata na kusindika
samaki mara baada ya kutembelea viwanda vya Vicfish, Kagera Fish na Mapanki
Company Limited.
Aidha Mhe. Kamani akiwa Kianga
Wilayani Karagwe alitoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Kagera kutumia fursa
iliyopo ya hali nzuri ya hewa, maji na ardhi kuanzisha ufugaji wa kisasa hasa ng’ombe na kuachana na migogoro kati ya
wakulima na wafugaji ya kupigania ardhi mara kwa mara .
Waziri Kamani alisema serikali
itawanyanganya vitalu wawekezaji wote waliopewa vitalu hivyo na wao kuvikodisha
kwa wafugaji kutoka nje ya nchi bila kuvitumia wao wenyewe. “Ardhi ya Tanzania
ni mali ya watanzania tu na siyo watu toka nje ya nchi.” Alististiza Waziri
Kamani.
Vilevile Waziri Kamani
aliwahakikishia wananchi kuwa wizara yake imejipanga kuhakikisha inamaliza migogoro ya wakulima na
wafugaji ili sekta ya mifugo iweze kukuza uchumi wa nchi kwa kuvutia wawekezaji
kuwekeza kwa wingi katika sekta hiyo.
Akitembelea ranchi za Kikulula
Karagwe na Kagoma Muleba na kuongea na wawekezaji waliowekeza katika vitalu
vinavyopatikana katika ranchi hizo alisema wanatakiwa kundeleza vitalu vyao na
kufuga ufuji wa kisasa ili kukidhi mahitaji ya nyama katika masoko ya ndani na
nje ya nchi.
Tayari kuna mwekezaji ambaye
anajenga kiwanda cha kusindika nyama katika ranchi ya Mabale Wilayani Missenyi
na kiwanda hicho mara baada ya kukamilika kitakuwa kinachinja ng’ombe 300 kwa
siku na kusindika ngozi kwa ajili ya bidhaa mbalimbali zitonanazo na ngozi
hizo.
Waziri Kamani pia alisema
serikali inakusudia kukiboresha chuo cha mifugo ambacho kimeanzishwa cha
Kikulula Wilayani Karagwe na kukifanya kuwa Chuo cha Kisasa nchini kwani bado
kina fursa kubwa ya ardhi.
Mhe. Kamani akiwa chuoni hapo alisema,
“Tanzania vyuo vya mifugo vipo saba tu, na kwasasa taifa linahitaji wagani wa
mifugo17000 waliopo ni 5000 tu, vyuo vinazalisha wagani 2500 tu, kwa hiyo chuo
hiki kikiboreshewa miundombinu kitaweza kudahili wanafunzi wengi zaidi.”
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2014