BALOZI KAMALA AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA TAASISI YA UWEKEZAJI NA BIASHARA YA BRUSSELS
Balozi wa Tanzania Belux na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi
ya Uwekezaji na Biashara ya Brussels Bi. Benedicte Wilders (kushoto) na
Mkurugenzi wa Idara ya Kimataifa wa taasisi hiyo Bwana. Philip Feytons.
Balozi Kamala amekutana na viongozi hao leo hii Brussels kuwaomba
wahimize makampuni ya Brussels kushiriki ziara ya kibiashara
inayoandaliwa kufanyanyika Tanzania mwishoni mwa mwaka huu.