BALOZI KAMALA ASHUKURU BENKI YA MAENDELEO YA ULAYA KWA MIKOPO NA MISAADA INAYOITOA KWA NCHI ZA AFRIKA, KARIBIANI NA PASIFIKI (ACP)
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi
wa nchi za ACP Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akishukuru Benki
ya Maendeleo ya Ulaya (EIB) kwa kutoa mikopo ya gharama nafuu na
kusaidia Maendeleo ya nchi za ACP. Balozi Kamala ameitaka Benki hiyo
kuongeza kiwango cha mikopo inayotoa katika nchi za ACP kutoka asilimia
10 ya mikopo inayotoa sasa hadi asilimia 20. Kamati ya Mabalozi wa nchi
za ACP leo imekutana na Uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Ulaya,
Luxembourg kubadilishana mawazo jinsi ya kuboresha utendaji wa Benki na
kuweka vipaumbele vya maendeleo na ushirikiano kati ya nchi za ACP na
Benki ya Maendeleo ya Afrika.