Bukobawadau

FUTARI NYUMBANI KWA MAMA AULAT OMARY 'BUYEKELA-BAKOBA' MJINI BUKOBA JULY 26,2014

Nyumbani kwa Mama Aulat Omar pichani kushoto,Wadau wameweza kushiriki chakula cha futari iliyo andaliwa na Mwanae Voguee Aziz Omary (kulia) ikitanguliwa na Dua iliyo ongozwa na Ustaadh Kamaru pichani katikati.
Kama ilivyokawaida wadau wamefungua kwa tende na maji, halafu ikafuata swala ya magharibi na baada ya hapo futari ikasogezwa mahala pake
 Sehemu ya Wadau pichani wakiendelea futari iliyo andaliwa na Kijana Voguee Aziz Omary nyumbani kwa Mama Yake Mzazi 'Mama Aulat Omar wa Buyekela Mjini hapa


Wadau wakiendelea kupati futari ya pamoja ikiwa ni vyakula aina mbalimbali  sambusa, nyama na mikate,wali,chapati,naona tambi za aina mbalimbali ,zenye ladha na maumbo tofauti
 Wakiendelea kupata futari
 Ustaadh Kamaru,Kijana Ash K Bin Amar (kati) na Ndugu Moa wakiendelwa kupata futari
 Sehemu ya Waumini wakipata futari iliyo andaliwa na KijanaVoguee Aziz Omary
Sehemu ya Waalikwa anaonekana Bi Faridah Mussa pichani (kulia)Dada Wilelimina na Mwanadada Idaiya pichani katika wakiendelea kupata futari.
 Sehemu ya wanadada wakiendelea kufurahia futari
 Ndugu Yusuph Mawella kama anavyo onekana
 Hakika ni mchanganyiko wa  futari yenye  Muhogo wa nazi Vipopoo pembeni kuna Keki, Juice ya passion nakadhalika yaani Shidaaaah!
 Kulia kabisa ni Kijana Herry Nuru.
 Mdau Moa akiteta na Ndugu Peter wakati anaendelea kupata futari,
  Namuona Mwanadada Zuleikh pichani katikati akiteta na Kish Kish wakati Bi Devotha anasikilia hii ni baada ya kupata vitafunwa , Uji na Juice.
 Kijana  Aziz,Mama Aulat (katikati)na Mama yake mkubwa Shekhat Aziza pichani kulia
 Sehemu ya Wadau walioweza kushiriki katika iliyo andaliwa na Kijana Voguee Aziz Omary nyumbani kwa Mama Yake Mzazi 'Mama Aulat Omar wa Buyekela Mjini Hapa
 Kijana Voguee Aziz Omary pichani kulia, akiwa na kinadada walioweza kushiriki Chakula cha futari  nyumbani kwa Mama Yake Mzazi 'Mama Aulat Omar wa Buyekela Bakoba.
 Mwanadada Jess Jane akiendelea kupata futari, na kufanyiwa Ukodak na Ndugu Yusuph Mawella.
 Mara baada ya kupata furahi,Zoezi la Ukodak likaendelea
 Sehemu ya Waalikwa katika hili na lile
Mama Aulat Omar akifurahi na Wageni wake.
 Katikati ni Bi Aidah Omar Mdogo wake na Voguee Aziz Omar akifuatiwa na Kijana Mkhusini.
  Marafiki wa Kijana Voguee Aziz Omary wakibadilishana maewazo mara baada ya futari.
 Mwanadada Vanny pichani kushoto na Kijana Ash K Bin Amar
Baada ya tukio Mama Aulat  akitoa neno la shukurani kwa wote walioshiriki katika futari.


Next Post Previous Post
Bukobawadau