MKURUGENZI WA SEKRETARIETI YA DUNIA YA NISHATI AKUTANA NA BALOZI KAMALA
Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Dunia ya Nishati Bwana. Steivan Defilla
(kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania Jumuiya ya
Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) baada ya kumaliza kikao
ofisini kwake. Kulia ni Bwana. Nodal Tayel Mratibu wa Taasisi hiyo.
Ujumbe huo ulifika Ubalozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya, Brussels
kueleza faida za nchi kuwa mwanachama wa Taasisi ya Nishati Duniani.