Bukobawadau

RWAMISHENYE 'OUT'!!MAKIRIKIRI TUNATISHA!!

 Uwanjani Kaitaba Maelfu ya Wananchi wameweza kujitokeza kushuhudia mtanange wa Soka michuano ya Kagasheki Cup hatua ya robo fainali.
 Ambapo timu ya Kitendaguro maarufu kwa jina la' Makirikiri'wamefanikiwa  kuwaondoa Rwamishenye kwa penati 7-6 na kutinga nusu fainali baada ya kwenda sare ya 0-0 dakika 90 za mchezo wa robo fainali.
 Tayari mpira umeanza, makirikiri wakiwa na Jezi yao ya Brazil 
Mchezaji wa Rwamishenye anafanyiwa madhambi.
 Mpira ukiendelea Uwanjani
 Kwa “ukali”na “ustahiki” wa mechi hii ndivyo wanavyo onekana Mashuhuda pichani Ndg Al Amin na Optaty
 Katika benchi la ufundi la Timu ya Rwamishenye.
 Wachezaji wa Benchi Timu ya Rwamishenye
 Sehemu ya mashabiki wakiendelea kufuatilia mchezo huu.
Hakika ni vigumu kuelezea kwa Taswira yanayojili Michuano ya Kagasheki Cup 2014
 Kagasheki Cup ni ligi  yenye msisimko /upinzani na kupendwa sana na Wakazi wa Mji wa Bukoba.
Katika hali ya umakini .
Kushoto ni 'Super Star' Mwinyi Kheeir kiongozi wa Timu ya Miembeni ambaye kwa sasa Jina lake linamake headline baada ya kuwaondoa kijemedali Wana wa Kashai , anafuatia Bwana Jamal Jamco Kalumuna na waliovalia 'ki -Obasanjo'ni Kijana Byshira na Shafih.
 Hadi dakika  90 matokeo ni  0-0 wanaonekana kutokusomeka mashabiki wa Rwamishenye pichani.
 Wachezaji wa Kitendaguro baada ya dakika 90 ya Sasa ni kuelekea hatua ya mikwaju ya penati
Ni kikosi Mahiri kinachonolewa na Kocha Mwalimu George.


Makirikiri katika kupoza mwili kabla ya kuanza hatua ya matuta.
 Baada ya dakika 90 za mchezo ,muda mfupi kuelekea hatua ya matua.
 Wachezaji wa Rwamishenye wakipata maji kabla ya kuanza kwa hatua ya mikwaju ya penati
Mchezaji wa Rwamishenye akiwa tayari kupiga Penati
 Kipa wa Kitendaguro baada ya kuchambuliwa na mpira kutinga nyavuni.
 Naaam
 Kijana Ashiraf na Kijana Hashimu wakifuatilia mikwaju ya penati.


 Mafanikio ya wana wa Makirikiri yametokana na Ubora wa Golikipa wao pichani
 Sehemu ya Mashabiki Jukwaa 'A'wakifuatilia soka


 Katika hali ya Umakini anaonekana Kipa wa Makirikiri akiwa tayari kuokoa Jahazi
Kwenye kiti ni Abdulrazak Majid mtangazaji wa 88.5 Kipindi cha michezo Kasibante Fm Radio
 Watu full kubanana ndani ya Uwanja wa Kaitaba.
 Sehemu ya wapenzi na washabiki wa soka wakiwa wametulia pembezoni mwa Uwanja.
Katikati na Mohamed Hussein Msemaji wa Kagera Sugar.
 Macho ya kila ya shabiki yakielekea uwanjani 
Mashabiki kuelekea muda wa furaha kwa washindi na Majinzi kwa 
  Kipa wa Makirikiri  ananyanyuliwa juu kwa kumpongeza baada ya kuokoa Jahazi.
 Mashabiki wa Kitendaguro/Makiriri wakiendelea kufurahia Ubingwa wao.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa jioni ya leo Uwanjani kaitaba,matukio ya picha zaidi ya 200 tembelea katika ukurasa wetu wa facebook kupitia >Bukobawadau Entertainment Media
Next Post Previous Post
Bukobawadau