Bukobawadau

KUHUSU KAFULILA KUHOJIWA NA TAKUKURU JUU YA ESCROW

Na Mwandishi wetu
Mbunge wa Kigoma kusini David Kafulila amehojiwa na kuwasilisha  ushahidi wake kwa maandishi  kuhusu suala la tuhuma za wizi katika akaunti ya Tegeta Escrow huku akieleza sababu zake ni kwanini anataka Bunge lichunguze badala ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali na Takukuru
Kafulila ametoa andiko la kurasa saba kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru huku nakala zikitolewa kwa Spika wa Bunge na Mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za Serikali, ametoa maelezo akiambatanisha na vielelezo kadhaa juu ya tuhuma hizo.
“Nikichangia hotuba ya Waziri mkuu nilitaka uchunguzi  ufanyike kupitia kamati teule ya bunge kuhusu tuhuma zinazohusisha kiasi cha dola 270 Milion zilizopaswa kuwa ndani ya akaunti hiyo sanjari na zile dola 122 milion zilizokwishatolewa na kupewa kampuni ya PAP inayomilikiwa na mfanyabiashara” ilisema sehemu ya maelezo hayo.
Kafulila amesema ni kwasababu Takukuru ni chombo chenye jukumu zito lakini haina meno kukabiliana na rushwa zinazowakabili vigogo wa serikali kwani mwamuzi wa mwisho katika masuala hayo huwa ni ofisi ya DPP ambaye amekuwa akitupilia mbali mashtaka kwa kisingizio cha mamlaka aliyonayo kikatiba.
Kwa mujibu wa barua hiyo ni Malalamiko ya Ofisi ya Takukuru yenyewe kusema kuwa ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini inakwamisha ufanisi wa vita dhidi ya rushwa ilikuwa ni ushahidi tosha wa yeye kukataa uchunguzi ufanywe na Takukuru.
Next Post Previous Post
Bukobawadau