TAARIFA ZA MSIBA WA DADA BERTHA GYALENGA MAARUFU KAMA (MREMBO)
Taarifa zilizotufikia Jioni ya leo Alhamis July 24,2014 kuwa Dada yetu ,rafiki yetu Bertha (Mrembo) Gyalenga amefariki Dunia katika hospital ya Mkoa Kagera.
Marehemu Bertha Gyalenga maarufu kama (Dada Mrembo) ni Mtoto wa Mwalimu Gyalenga na Marehemu Mzee Gyalenga zamani Mkurugenzi RETCO Kagera.
Timu nzima ya Bukobawadau Blog inatoa pole kwa familia, Ndugu,jamaa na marafiki kwa kuondokewa mpendwa wetu!
R.I.P dada yetu mpendwa, tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi!!