TISHIO UWANJA WA NDEGE WA ENTEBBE
Ubalozi wa Marekani nchini Uganda umetoa onyo ukisema kuna "tishio dhahiri ... kutoka kundi lisilojulikana" kushambulia uwanja wa ndege wa Entebbe. Onyo hilo limechapishwa kweye tovuti ya ubalozi huo kufuatia tahadhari nyingine iliyotolewa na mamlaka za Marekani siku ya Jumatano ya kuimarisha ulinzi katika viwanja vya ndege vya Mashariki ya Kati na Ulaya vyenye ndege za moja kwa moja kwenda na kutoka Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa za kiuchunguzi, kuna tishio thabiti kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe leo kati ya saa tatu usiku hadi saa tano- imesema taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa za kiuchunguzi, kuna tishio thabiti kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe leo kati ya saa tatu usiku hadi saa tano- imesema taarifa hiyo.