Bukobawadau

UJERUMANI MABINGWA KOMBE LA DUNIA 2014 (BAO LA SUPER MARIO GOTZE Dk. 113 EXTRA TIME )

Nini wao ni kucheza Mchezaji wa zamani wa Hispania Nahodha Carles Puyol akiwa na Mwanadada Gisele Bundchen ambaye ni mwanamitindo wakizungusha Uwanjani  Kombe la Dunia  muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali
 Mashabiki wa Argentina wakiwa tayari kwa ajili ya mchezo wa fainali.
Lena Gercke ambaye ni mpenzi wa Mchezaji wa Ujerumani Sami Khedira, akiwa tayari kusubiri mchezo wa fainali ya kumbe la dunia
Katikati ni mshambuliaji wa Ujerumani Miroslav Klose akijaribu kukatiza ngome ya Mchezaji wa Argentina Javier Mascherano
Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi (kushoto) akijaribu kumfukuzia beki wa Ujerumani Mats Hummels
Chini ni Mchezaji Christoph Kramer baada ya kupata suluba za Uwanjani
Christoph Kramer wa Ujerumani anapata matibabu muda mfupi kabla ya kubadilishwa
Mwanzoni mwa kipindi cha kwanza beki wa Ujerumani Benedikt Howedes (wapili kulia) anaruka juu na kupiga kichwa ,mpira akagonga mwamba na kuwa salama ya Argentina
 Shabiki aliye vamia Uwanjani na kujaribu kutoa Busu kwa nia njema na ishara ya upendo katika kumpongeza mchezaji Benedikt Howedes wa Ujerumani
 GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOAAAAALLL!!Mchezaji 113Mario Gotze anaipatia Ujerumani Bao la kwanza mnamo dakika ya 113 ya muda wa ziada (Extra time)
 Super Mario:Mchezaji wa  Ujerumani Mario Gotze  na Thomas Muller wakishangilia baada ya kufunga bao katika muda wa ziada GERMANY 1-0 Argentina
 Ni kama mchezo umefika mwisho, pichani anaonekana Argentina Lionel Messi na Sergio Aguero (kulia) wakipata mawazo wakati wa kuweka mpira kati baada ya goli la mchezaji Mario Gotze wa  Ujerumani
  Shujaa wa Ujerumani Mario Gotze anasalimiana naLionel Messi baada ya mchezo wa fainali za  Kombe la Duni
 Pichani anaonekana  kocha wa Argentina Alejandro Sabella akiwa amesimama  mbele na wachezaji wake muda mchache baada ya mpira kumalizika
 Shangwe za mabingwa wa Kombe la Dunia , pichani ni Mchezaji Philipp Lahm akiwa amenyanyua  Kombe la Duniabaada ya kuwashinda Argentina 1-0 katika muda wa ziada 
 
Next Post Previous Post
Bukobawadau