UVUTAJI BANGI RUKSA SASA WASHINGTON
Uuzaji wa bangi kama ulevi wa starehe
utaanza kuuzwa rasmi hii leo katika jimbo la Marekani la Washington.
Hili ni jimbo la pili nchini humo kuhalalisha bangi kwa matumizi ya
burudani, baada ya jimbo la Colorado kufanya hivyo. Mapato ya kodi
kutokana na uuzaji wa bangi katika jimbo la Colorado yamefikia dola
milioni kadhaa sasa.
Mchakato huo utadhibitiwa kwa makini katika jimbo la Washington. Maduka ishirini na tano tu ndio yamepata leseni ya kuuza mpaka sasa, ingawa maafisa wanasema idadi hiyo huenda ikaongezeka na kufikia maduka takriban mia moja. Majimbo mengine 23 nchini Marekani tayari yanaruhusu uuzaji na ununuaji wa bangi lakini kwa sababu za kitabibu.