WAWEKEZAJI WAANZA KUITIKIA WITO WA KUWEKEZA MKOANI KAGERA
Mkoa wa Kagera umekuwa ukifanya juhudi kabambe za kujitangaza na kuzitangaza fursa zake mbalimbali za uwekezaji ili
kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza mkoani humo kwa nia
ya kuinua pato la mkoa pia kuinua uchumi wa wananchi kupitia ajira.
Juhudi hizo za mkoa wa Kagera
zimeanza kuleta matumaini baada ya wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi
kuanza kuonesha nia ya kuwekeza katika sekta mbalimbali za kiuchumi ikiwemo
kilimo cha kibiashara na kisasa pamoja na ufugaji wa ng’ombe wa kisasa.
Global International Agency ni
Kampuni mojawapo ya ndani ya nchi ambayo imeonyesha nia ya kuja kuwekeza mkoani
Kagera katika sekta ya kilimo cha kisasa cha kibiashara katika zao la shairi ambapo tayari kampuni
hiyo imeshapata maeneo ya kuanzia kilimo hicho katika wilayani Missenyi.
Kampuni ya Global International
Agency tayari imefanya utafiti wa kutosha katika mkoa wa Kagera kuhusu ustawi
wa zao la shairi na imeonekana hali ya hewa pamoja na aina ya udongo vinafaa
sana kustawisha zao la shairi.
Utafiti huo umefanywa katika
Wilaya Missenyi na tayari maeneo ya kulima zao la shairi ya mepatikana katika
kata ya Bugolola kwenye vijiji vya Bugolola, Buchulago na Kabingo pia kata ya
Mushasha katika kijiji cha Bulembo.
Global International Agency baada
ya kupata maeneo hayo katika Wilaya ya Missenyi inaendelea na utafiti katika
maeneo mengine ya mkoa wa Kagera ili kupata maeneno mengi zaidi. Aidha
inaendelea na utafiti jinsi ya kushirikisha wananchi katika kilimo hicho kwa
kuwanufaisha bila kuwanyonya.
Akiongea katika kikao na uongozi
wa mkoa wa Kagera Kuhusu soko la shairi Mkurugenzi Mtendaji wa Global
International Agency alisema kuwa zao la shairi lina soko kubwa kwani pamoja na
kutumika kutengeneza pombe (Beer) lakini plastiki kama chupa za maji na ndoo
pia mabaki hutengeneza kartasi.
“Tanzania Breweries Limited
(Kampuni ya kutengeneza Bia Tanzania TBL) inapata asilimia 25 ya shairi kutoka
Tanzania na asilimia 75 ni kutoka nje ya nchi jambo ambalo linaonyesha
uhuhitaji shairi katika soko.” Alisistiza Fidelis Bashasha Mkurugenzi Mtendaji
Global International Agency.
Uwekezaji katika kilimo cha
shairi mkoani Kagera utfungua fursa nyingine nyingi katika uwekezaji kutokana
na zao la shairi kutengeneza vitu vingi kama plastiki mfano chupa za maji,
ndoo, viti na beseni. Aidha masalia yake
hutumika kutengeneza karatasi pia shairi hutumika kutengeneza chakula kama
mikate.
Kutoka na hali hiyo kilimo cha
shairi kikifanikiwa mkoani Kagera wawekezaji wa kutengeneza bidhaa mbalimbali
za plastiki watakuja kuanzisha viwanda hapa mkoani Kagera kikiwemo kiwanda cha
kutengeneza karatasi kwani malighafi itakuwa inapatikana kwa urahisi.
Kampuni ya Global Internationa
Agency wanahitaji hekari 100,000 za ardhi ili kuzalisha zaidi ya tani 100,000 za shairi ili kukidhi
soko la ndani nje ya nchi. Pia uwekezaji mara utakapoanza wananchi 8700
wanatarajia kupata ajira kwa kuanzia.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa
Kagera Bw. Richard Kwitega aliipongeza Kampuni ya Global International Agency
kwa kukubali kuwekeza katika mkoa wa Kagera na kuwaomba pia wasiishie katika
wilaya moja ya Missenyi bali wazifikie Wilaya zote za Mkoa wa Kagera.