Bukobawadau

YALIYOJILI UWANJANI KAITABA #MIEMBENI 1-1 RWAMISHENYE #KAGASHEKI CUP 2014

Jukwaa kuu pichani kushoto ni Ndg Juma chama Umande katibu wa TFF Mkoa Kagera na kulia kwake ni Haji Abdul Sued Kananga ambaye ni Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Mh. Balozi Kagasheki.
 Sehemu ya mashabiki wakiwa wamesimama usawa wa Lango Kuu,kuingia Kaitaba
 Wachezaji wa Rwamishenyi wanatumia nguvu akili na kasi  kuakikisha wanapata ushindi
 Noma ni pale mambo ya ' Brazuka 2014  yanapo hamia Kaitaba
 Mchezaji wa Rwamishenyi jezi namba 6 anajaribu kunyanyuka Uwanjani wakati anendelea kumkanyaga kwa makusudi Kiungo wa Miembeni kama alivyo naswa na Camera yetu!
 Miembeni wanaongoza kwa Bao Moja lililopatikana mwanzoni mwa kipindi cha kwanza.
 Timu zote zinajaribu kuwa makini na kuonyesha kuwa kuna kitu wanacho kihitaji
 Mwamuzi anatoa Kadi ya njano kwa Mchezaji wa  Miembeni aliyejiangusha kwa makusudi.
 Mlinda Mlango wa Rwamishenye anashangazwa na kishindo cha ghafla wakati anajiandaa kupanga mpira,Ni pale anapojiangusha pasipo sababu Mshambuliaji wa Miembeni pichani (kushoto)
 Sehemu ya Wadau kutoka Bukoba Cable Tv wakifuatilia mechi kwa ukaribu.
 Jukwaa la Mashabiki wa Timu ya Rwamishenye
Wadau wakiendelea kufuatilia soka Uwanjani Kaitaba.
 Mnazi mkubwa wa Bilele Fc.
 Vijana mashabiki wa Rwamishenye ikiwa timu yao iko nyuma kwa Bao moja.
 Sehemu ya mashabiki jukwaa la mchanganyiko
 Mashabiki wakiendelea kufuatilia Soka
 Mpira ni Mapumziko Miembeni wanaongoza dhidi ya Rwamishenye 1-0
 Mshambuliaji wa Miembeni pichani
 Wachezaji wa Miembeni Fc.

 Wachezaji wa Rwamishenye wakielekea katika chumba cha mapumziko
 Batuache Sisi bi balaa!! ndivyo linavyo someka bango la Shabiki wa Rwamishenye
Waamuzi wa Mchezo wa leo July 10,2014 Ikiwa ni Muda wa mapumziko
 Mpaka muda wa mapumziko Miembeni wanaongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Rwamishenye.
 Anaonekana Mchezaji Kiungo mkabaji wa Timu ya Miembeni Sadick Athmani Sadick (Kafuka)
 Mbele ya Camera yetu ni Ndg Moa Nyundo , kiongozi wa Timu ya Kashai
 Wapenzi na washabiki wa michuano ya Kombe la Kagasheki Uwanjani Kaitaba
 Mohamed Kassim pichani katikati mchezaji Bukoba Veterans
 Anaonekana Mdau Nuru Kasabi, Mnazi wa Fc. Bilele
 Katika hili na lile, kulia ni Kijana Obrah Karugira wa Abanyaluganda wa Kashai
 Sehemu ya Mashabiki Jukwaa Kuu
 Taswira mbalimbali Uwanjani Kaitaba  ikiwa ni muda wa mapumziko.
 Kipindi cha lala Salama kinaendelea Uwanjani
 Picha zaidi na matukio mengineyo  ya Michuano ya Kagasheki Cup 2014 yanapatikana kila siku katika ukurasa wetu wa facebook
 Panatokea zogo baada ya mchezaji wa Rwamishenye kufanyiwa madhambi.
Moja kati ya picha isiyo someka.
 Rwamishenye wamerejea kipindi cha pili kwa kasi ya aina yake
 Na hi nduyo picha yetu  bora kwa kutwa nzima ya leo Alhamisi ya tarehe 10 July 2014
 Dakika ya 78' Rwamishenye wanapata bao la kusawazisha na kufanya matokeo kuwa 1-1
 Hakuna maneno ya kueleza namna upande wa pili ulishangazwa na bao hilo
 Wachezaji wa Rwamishenye wanarudi Uwanjani  baada ya kushangilia bao lao.
 Haya ndiyo yaliojili Uwanjani Kaitaba jioni ya leo Alhamisi ya tarehe 10 July 2014
Mpaka Mwisho Miembeni 1-1 Rwamishenye #Kagasheki Cup 2014


Next Post Previous Post
Bukobawadau