Bukobawadau

BILELE MABINGWA MKOA MASHINDANO YA 'SAFARI LAGER NATIONAL POOL CHAMPIONSHIP 2014'

 Timu ya Bilele Pool Club imeweza kunyakua ubingwa wa Mkoa katika mashindano ya Pool Taifa yajulikanayo kama “ Safari Lager National Pool Competition 2014.”yanayo dhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania  (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo 
 Bingwa wa  mkoa kwa upande wa timu amepata Sh.800,000 kutoka Sh.500,000 ya msimu uliopita, mshindi wa pili Sh.400,000, mshindi wa tatu Sh.250,000.TBL mwaka huu wameamua kuboresha mashindano ili kuongeza hamasa  na changamoto kwa vilabu  kwa kuongeza zawadi asilimia 15% .
 Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume), bingwa amepata Sh.400,000, mshindi wa pili Sh.250,000, wakati bingwa kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanawake), atapewa Sh.300,000 na mshindi wa pili Sh.200,000.
 Mchezaji wa Hamugembe pichani akifuatilia mchezo dhidi ya mpinzani wake
 Fainali za kitaifa za 2014 za “Safari National Pool Competion” zinatarajiwa kufanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa kushilikisha Mikoa 17 
 Taswira mchuano ukiendelea.
Mashindano ya  mchezo wa pool ya ‘Safari Lager National Pool Championship 2014’, ngazi ya mikoa yalianza Juni 14, mwaka huu katika mikoa 18 ya Tanzania Bara.
 Bi Justine  Charles mshindi wa pili upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanawake)
 Mgeni Rasmi Ndugu Jacob Kilianga anamkabidhi mshindi wa pili Sh.200,000.
Pichani anaonekana Bi Sajida Said mara baada ya kutangazwa kuwa bingwa wa Mkoa kwa upande wa (wanawake) na kujipatia zawadi ya Tsh Sh.300,000/
 Bi Sajida Said  bingwa kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanawake), mra baada ya kukabidhiwa Sh.300,000 
Wachezaji 4 walioshiriki kama mchezaji mmoja mmoja (wanaume) wanapata kifuta machozi cha sh 50,000 Elfu hamsini
 Ndugu Msomi Njagi Mchezaji kutoka timu ya 'Mnyonge 'anakabidhiwa  Sh .50,ooo/-
 Mchezaji Jabir Daudi anajipatia Sh.50,000 kwa kushiriki upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume)
 Mshiriki mwingine ni Alex Emmanuel 
 Alex Emmanuel akionyesha zawadi yake  kwa mashabiki mara baada ya kukabidhiwa
Mchezaji wa 4 kupata zawadi kwa washiriki kama kifuta machozi ni Frank George
 Mchezaji Erick Patrick  akiwa tayari kukabidhiwa zawadi ya sh.100,000  kama mshindi wa nne upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume).
 Ozil Vedasto  Mshindi wa tatu kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume) anakabidhiwa zawadi ya SH.150,000
Mchezaji Ozil Vedasto  akihakiki hesabu yake mara baada ya kukabidhiwa.
Mshindi wa pili ni Mchezaji Hakimu Mzamilu kutoka Timu ya Bilele anajipatia Sh.250,000
 Mchezaji Robert Mutasingwa kutoka timu ya bilele ndiye Bingwa na mwakilishi wa Mkoa wa Kagera.
Robert Mutasingwa ndiye bingwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume),na mwakilishi wa Mkoa wa Kagera  anajipatia kitita cha sh Sh.400,000.
 Mwakilishi wa TBL Bukoba Ndugu Rackson Kahabuka  amesema Fainali za taifa za mashindano hayo yanayodhaminiwa na wadhamini wakuu wa mchezo huo nchini, Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kupitia bia ya Safari Lager, ambazo zitashirikisha mabingwa wa kila mkoa, zitafanyikia mkoani Kilimanjaro.
Baada ya taarifa kutoka kwaMwakilishi wa TBL Bukoba Ndugu Rackson Kahabuka, hatua inayofuata ni kukabidhi zawadi kwa timu yaana Club zilishoshiriki, pichani ni Kapten wa timu ya Quality Pool Center.ambao ni washindi wa nne, akikbidhiwa kitita cha sh.150,000.

 Mshindi wa Tatu ni Bukoba Pool ambao wanajinyakulia sh.250,000.
Timu Kaptein wa Bukoba Pool mara baada ya kukabidhiwa kitita cha sh 250,00 
 Zawadi kwa mshindi wa pili Sh.400,000 ambao ni Hamugembe.
  Kutoka kampuni ya InterGrated pichani  ni msimamizi wa mashindano hayo Ndg Livingstone
 Viongozi wa Juu timu ya Bilele wanapanda jukwaani
Tayari ni Sheeedah viwana vya Q Bar  mashabiki wa Bilele wakiserebuka!

Kabla ya Zawadi kutolewa kwa Mabingwa wa Mkoa,Wanapanda jukwaani viongozi wa timu hiyo.
Wachezaji wa Bilele wanapanda  jukwaani tayari kwa kukabidhiwa zawadi kama Mabingwa Mkoa
Kapten wa timu ya Bilele anakabidhiwa SH 800,000/- laki nane  za kitanzania.
 Nahodha wa timu Bilele akifanya yake kwa kuzitandaza noti 
Wachezaji na Mashabiki wa Bilele wakishangilia  mara baada ya kumalizia mchezo wa mwisho na wa ushindi dhidi ya Hamugembe.
Ndivyo mambo yalivvyokuwa mara baada ya Bilele kutwaa Ubingwa na kuwa wawakilishi wa Mkoa.
 Muonekano wa Mashabiki.
Taswira mbalimbali kutoka viwanja vya Q Bar.
 Mikoa iliyoshiriki mashindano hayo kuwa ni pamoja na mikoa maalum ya kimichezo ya Kinondoni, Ilala, Temeke, Pwani, Marogoro, Dodoma, Tanga, Lindi, Manyara, Mbeya, Kilimanjaro, Arusha, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Kagera na Iringa.
Mpaka hapo BUKOBAWADAU BLOG hatuna la ziada tukiripoti moja kwa moja fainali za mashindano mchezo wa Pool kwa ngazi ya mkoa  mpaka Taifa uliofanyika jana  kwenye Ukumbi wa Q Bar

Next Post Previous Post
Bukobawadau