Bukobawadau

MATANGA YA BI THERESIA K.LAURENT 'KIMILA' ZAIDI

 Sehemu ya Watoto wa marehemu Bi Theresia na ndugu wa familia waliojifunga Shuka/kitambaa Cheupe hapa wakiwa tayari kuwasikiliza Wajukuu wa Marehemu ikiwa ni kitendo maalum cha 'Okusilibya' kwenye msiba wa Bibi yao
 Wajukuu wa Marehemu Bi Theresia wakiendelea kuigiza 'OKUSILIBYA'enzi za maisha ya uhai wa Bibi yao kutokana na mila na desturi za kabila la Wayahaya  'Okusilibya' ni kitendo ambacho kwa kawaida ufanywa na  wajukuu wakiume na  wakike huku wakipiga ngoma na kuimba  nyimbo mbali mbali ,shughuli inayomalizika kwa malipo pale wanapo watoza kiasi cha fedha ndugu wa ukoo na watoto wa mtu aliyefariki. 
Wajukuu wakiendelea kuwajibika.
Mkusanyiko wa vitu mbalimbali kulingana na taratibu zilizopo.
Msemaji wa Familia , Mwl.Leonidas Kagirwa akionyesha kulielewa somo la Wajukuu.
Sehemu ya wajukuu waliokuwa wakikabiliwa na shughuli maalum ya 'Okusilibya'wanatoka nje kwa nyimbo mbali mbali 
 Wajukuu waleeee... na Ngoma  zao,hatua hii inakuwa ya mwisho ikiwa ni siku ya kuanua matanga.
Wajukuu wa Marehemu kwa utaratibu  maalum ukusanya vitu mbalimbali  vikiwa vimefungwa kwa pamoja na vitu vingine kama jembe na kuviweka juu ya kaburi 
Wakati yale yakiendelea Ndani, upande wa nje mambo yako hivi.
 Wanaonekana Sehemu ya waombolezaji katika shughuli hii ya matanga.
 Anaonekana Ndugu Justuce Rugaibula akiwa karibu sana familia hii ,kutokana na Urafiki aliokuwa nao na Marehemu Lutta (Theonist Tutashoborwa)
Ndugu Justuce akishiriki katika msiba huu wa Mama mzazi wa aliyekuwa rafiki yake marehemu (Theonist Tutashoborwa), anaonekana pichani  akisalimiana na kuwakaribisha waliofika kushiriki shughuli hii ya  matanga ,anapeana mkono na Ndugu Japhet Katalaiya familia ya Katalaiya pia ina nasaba na familia ya Marehemu Bi Theresia Kokwikiriza Laurent.
 Muda wa kushiriki Chakula katika shuhuli hii yenye msamiati wa neno ' Matanga'
 Watu wakiendelea kupata Chakula katika matanga ya Bi Theresia K. Laurent
 Hakika kimeandaliwa  chakula kizuri pamoja na vinywaji

 Utaratibu wa huduma ya Chakula ukiendelea.
 Wanafamilia wakifuatilia utaratibu mzima kwa ukaribu.
 Shughuli ya matanga ni kama sherehe za kitamaduni.
 Sehemu ya wadau wakiendelea kushiriki zoezi la kupata mulo.
 Ndugu Nelson na Dada Mery
Wadau wakipata msosi.
 Moja ya kivazi tulichokutana nacho mkyalo!!.
 Mdau Beneth Katika hili na lile.
 Anaonekana Mdau pichani akitafakari jambo.
 Mbele ya Camera yetu ni Mdau tuliyekutana naye huko Kijijini Bukabuye anayejishughulisha na huduma ya Viti na Matent ya kukodishwa.
 Watoto wakitembezewa Vinywaji
  Kama kawaida Densi huchezwa katika sherehe za kitamaduni kama vile matanga
Kufikia majira ya saa mbili Usiku hali ilikuwa hivi.
Watu wanakula Kadansee...
PICHA ZAIDI INGIA HAPA>>Bukobawadau Entertainment Media
Next Post Previous Post
Bukobawadau