Bukobawadau

MIEMBENI WATWAA UBINGWA KAGASHEKI CUP 2014

TIMU ya Kata ya Miembeni mitaa ya Uzunguni Bukoba LEO imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa michuano ya kuwania Kombe la Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini KAGASHEKI CUP 2014 baada ya kuinyamazisha Makirikiri wana wa kitendaguro kwa kuilaza mabao 2-1 katika pambano kali la fainali ya michuano hiyo.
 Bao la kwanza la Miembeni lime wekwa kimiani na Mchezaji mahiri Babu Ally pichani,mnano dakika ya 72  ya mchezo na dakika sita baadae kwenye dakika 78 kutupia tena bao la pili kwa njia sawa na ya kwanza kwa kuachia kombora midhiri ya 'Choop' ile wahaya wanahita 'Entonyeza' kutokana na mipira ya 'free kick'.
 Ushindi huo ulioshuhudiwa na Mgeni Rasmi Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki,Afisa Utamaduni Manispaa Bukoba ,watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ,Waheshima Madiwani na Viongozi wa Bukoba Veterans.
 Mchezo ukiendelea Uwanjani.
Mlinda mlango wa miembeni
 Mpaka mapumzika timu zote zimeenda sare ya bila kufungana 0-0.
 Mgeni Rasmi Mh. Balozi Kagasheki pichani kushoto, akifuatiwa na Mh. Abdul Sued (Kananga) na wa mwisho kulia ni Ndugu Al masoud Kamala.
 Mh.Jeanifer Murungi Kichwabuta na Ndugu Self Mkude.
 Mh. Yusuph Ngaiza Diwani Kashai
 Mashabiki wa Kitendaguro wakiendelea kupasha na ngoma zao!!
Taswira Uwanjani
 Mgeni Rasmi Balozi Khamis Kagasheki Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini akiongea na mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya michuano hii Ndugu Hamimu Mahamud pia ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Kagera.
Warembo waliohusika na kulitembeza Kombe,kabla alijakabidhiwa kwa Mabingwa .
Ndivyo Gari la miembeni linavyo endelea kuchukua kasi...kuukalibia ubingwa.
 Mdau Jamal Jamco Kalumuna akishangilia bao la kwanza la Miembeni .
 Wachezaji wa Miembeni wakiendelea kushangilia bao .
 Mshambuliaji wa Miembeni Mtaalam Babu Ally akisema na mashabiki baada ya kutupia bao la pili.
Mfungaji Babu Ally, uso kwa uso na mashabiki wa Miembeni

Kijana Obeid shabiki wa Miembeni akiwa kajiachia na Mamsapu pembeni
 Mohamed Kassim mnazi wa Timu ya Bilele iliyo ondolewa na Miembeni hatua ya robo fainali.
 Katikati ni Said Mshamu Kitonsa, mchezaji zamani RTC Kagera
 Kutoka 88.5 Kasibante Fm Radio ni watangazi Jeromo na Abdulrazak Majid
Mdhamini ya Michuano ya Kagasheki Cup 2014Balozi Khamis Kagasheki ambaye ni Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini akiongea machache na wananchi waliojitokeza Uwanjani Kaitaba kushuhudia mechi ya fainali.
Maelfu ya Wananchi wakimsikiliza Mbunge wao Balozi Khamis Sued Kagasheki.
Mh. Balozi Kagasheki akiendelea kutoa ufafanuzi kuhusiana na Michuano hii.
 Mtu wa watu , Mdau Enock akimsikiliza Mh. Balozi Kagasheki kwa mbali
Msimamizi na mwendazaji wa Michuano ya Kagasheki Cup ndg Malick Sudi Tibabimale akitolea jambo ufafanuzi.
Taswira uwanjani Kaitaba muda mchache kabla ya kutolewa zawadi.
 Mh.Kagasheki akikabidhi zawadi ya Tsh 200,000 kwa mfungai bora wa michuano hii.
 Mchezaji Odilo wa timu ya Kashai ndiye mfungaji bora wa Michuano ya Kagasheki Cup 2014
Mchezaji Chipukizi wa Mashindano haya akisalimiana na Mh. Balozi Khamis Kagasheki .
Mchezaji Chipukizi anapata zawadi ya Baiskeli na Pesa taslim  Tsh 100,000/-(laki moja)
Sehemu ya mashabiki wakifuatilia kinachojili.
 Mshindi wa tatu anapata zawadi ya Tsh 1,500,000/- pichani ni Kiongozi wa Bilele ndg Mohamed Kassim na kitita cha Shilingi milioni moja na nusu
 Mh.Balozi Khamis Kagasheki Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini pia alidhamini mechi kati ya Bukoba Veterans na Madreva Tax,mechi ambayo madreva Tax waliwatembezea kichapo Bukoba Veterans.
Kiongozi wa Bukoba Veterans Ndg Mwinyi mara baada ya kupokea zawadi ya Tsh. 200,000(lakimbili) kama mshindi wa pili kufuatia kufanyika kwa pambano kati ya Bukoba Veterans na Madreva Tax ambao wamejinyakulia kitita cha Tsh 300,000(laki tatu)
Mshindi wa pili anapata zawadi  ya Tsh 3,000,000/-(Milioni tatu)
 Kati wa Mbunge Ndugu Jumanne Bingwa akiteta jambo na Mh. Balozi Kagasheki
Mshindi wa Pili mara baada ya kukabidhiwa zawadi
Zawadi ya Mshindi wa pili Tsh 3,000,000(milioni tatu) na Medan za shaba pisi 25
Sasa ni Zamu ya Mabingwa wana wa Miembeni, Watoto wa mitaa ya Uzunguni na Nyamkazi, aka 'UTAIPENDA'
Mshindi wa Kwanza anajinyakulia Tsh 5,000,000/-(Milioni tano) na medali za dhahabu pisi 25.
Wachezaji na Viongozi wa timu ya Miembeni wakivalishwa Medali za zahabu kabla ya kukabidhi kombe .
 Mgeni Rasmi Balozi Khamis Kagasheki Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini na muandaji wa mashindano haya akikabidhi Kombe kwa Kapteni wa Timu  ya Miembeni
 Shangwe kwa wachezaji wa Miembeni mara baada ya kutawazwa kubwa Mabingwa wa michuano ya kuwania kombe la Mbunge.

 Katika ukodak Camera inakutana na Mwanadada G-Trezo Martin
 Unaambiwa mambo ni Bam Bam, Baba Anasi anasema ni 'Swadakta'
 Sehemu ya mashabiki wa Soka,Kijana Eddy naye yupo.

Mashabiki wa Miembeni pichani
 Haya ndiyo yaliyojili katika hitimisho ya Mashindano ya Kagasheki Cup 2014, Mashindano haya yamegharimu kiasi cha Tsh 35,000,000/-Milioni 30
 Jumla ya kata 14 zimeshiriki mashindano haya, kata 8 za ukanda wa Kijani (Green belt) zilipewa sh.500,000/-laki tano kila moja ambapo jumla yake ni Milioni 4(4,000,000) kwa ajili ya usajili au maandalizi.
Kiasi cha Sh.8,500,000 (milioni 8) imetumika katika aandalizi ya Kamati ya  Kagasheki Cup 2014.,Waamuzi  wa michezo hii wamepata laki nne (400,000)
 Mtiririko wa Zawadi kipa bora amepata  Tsh200,000/-( laki tano),Timu yenye nidhamu imepewa zawadi ya Tsh 500,00/-(laki tano) mchezaji Chipukizi zawadi ya Baiskeli na pesa taslimu Tsh 100,00/-(laki moja)
Upande wa Mchezaji bora mwenye nidhamu kapata Tsh 250,000/-(laki mbili na nusu)mfungaji bora Tsh 200,000 (laki mbili) Mshindi wa kwanza 5,000,000 na mshindi wa pili 3,000,000  nao washindi wa tatu wanapata 1,500,000 ambapo kiasi cha Milioni 8 kimetumika kwa ajili ya Sound uwanjani yaani Vyombo vya matangazo kwa kila mechi Uwanjani.

Mr Evance pichani kushoto akishow love na Mchezaji Babu Ally wa Miembeni.
Kiongozi wa timu ya Miembeni Mwinyi Kheir pichani kushoto akiwa na kombe mkononi


Kombe likizunguka Viunga vya Mji wa Bukoba, ambapo kesho litakabidhiwa rasmi kwa Viongozi wa Kata hiyo wakiongoza na Mzee Yusuph Mbagwa na Mh. Richard.
Next Post Previous Post
Bukobawadau