Bukobawadau

MISS LAKE ZONE 2014 KUONDOKA NA GARI

Mdhamini wa shindano la Miss Lake zone 2014 LEONARD BUGOMOLA, mkazi wa Mtaa wa Nyamalembo Wilayani Geita ambaye ni Mkurugenzi wa Lenny Hotel, akiwa na Walimbwende 18 akiwaonyesha gari alilotoa kwa ajili zawadi ya mshindi wa kwanza atakayeibuka kidedea mwishoni mwa mwezi huu.
Jumula ya Wanyange 18 wa Redds Miss Lake zone 2014 katika pozi moja matata.
Ndugu  Leonad Bugomola ambaye ni mfanya bishara mkoani Geita  pia mmiliki wa Lenny Hotel alisema kuwa ameamua kutoa zawadi hizo kutokana na Mwenyezi Mungu kumjalia kile alichonacho, pia ametoa shukrani kwa mmoja wa wafanyabiashara  mjini hapo Ndugu Thom Rweyemamu maarufu kwa jina la Desire kwa ushirikiano mkubwa anaotoa .
Naye Mkurugenzi wa Disire Lodge ndugu Thom Rweyemamu amesema mbali ya kupata gari, pia mshindi wa kwanza atakabidhiwa fedha taslimu katika Shindano hilo la Redds Miss Lake Zone 2014 linatalajiwa kufanyika Aug 30,2014.
 Muda mchache uliopita Ndugu William Rutta Meneja uendeshaji wa kampuni ya utalii ya Kiroyera,alipotembelea Kambi ya Mazoezi ya Redds Miss lake zone 2014.
Next Post Previous Post
Bukobawadau