SALA YA WANAJUMUIYA WA KYAZI-KAHORORO NYUMBANI KWA MAMA JUSTUCE RUGAIBULA
Awali ya yote Mama Justuce Rugaibula (pichani),pamoja na familia yake Wanamshukuru Mwenyezi Mungu kwa baraka zake.
Kwa Upendo wa Kristo ,katika kile kinacho aminika ni kumtumikia na kuwajibika,hapa ni nyumbani kwa Mama Justuce Rugaibula ,Padre anaungana na Wanajumuiya wa Kyazi Kata ya Kahororo Mjini Bukoba kwa kuongoza Ibada maalum iliyofanyika nyumbani hapo.
Huu ni utaratibu wa kawaida kwa Wakatoliki kumtukuza Mungu katika vipindi mbalimbali au ngazi kwa ngazi kupitia Jumuiya ndogo ndogo, vigango ama dekania.
Nipeni mioyo yenu iliyo wazi na iliyosafishwa, nami nitaijaza upendo
wa Mwanangu.Upendo wake utaipa maisha yenu maana nami nitatembea
pamoja nanyi;'hayo ni maneno kutoka katika maandiko'
Padre anaongoza maombi ya kuibariki nyumba hii.
Padre hapa akiendelea kuongoza sala kuwaombea Wanafamilia hii kwa siku hiyo
Maandalizi ya Maji ya baraka.
Padre akitoa Maji ya baraka kwa waumini
Maombi yakiendelea,Tuna kila sababu ya kumtukuza Mungu katika kipindi hiki na kinginecho.
Sehemu ya Wanakwaya na Waumini walioshiriki katika Ibada hiyo
Muonekano wa Waumini katika Ibada hiyo.
Padri akitoa mahubiri
Sehemu ya Waumini wakiendelea kumsikiliza Padri
Wanajumuiya wakikabidhi sehemu ya bidhaa.
Sehemu ya wanajumuiya na wageni toka sehemu mbalimbali wakati wa Ibada hiyo
Maandiko yanasema;'wataokoka tu wale ambao watatembea kwa upendo na imani kumwelekea Baba wa Mbinguni'
Wanakwaya wakitumbuiza Ngoma na vinanda vikisikika wakati wanakwaya wakitumbuiza katika Ibada maalum ya Wanajumuiya wa Kyazi-Kahororo iliyofanyika nyumbani kwa Mama Justuce Rugaibula.
Bukobawadau Blog tunazidi
kuwaombea ushirikiano katika vipindi vyote kwa Upendo naVitendo.
Nawakusanya kama mitume wangu na nitawafundisha jinsi ya kuwajulisha
wengine upendo wa na jinsi ya kuwafikishia habari njema.
Mama Justuce Rukaibula akitoa sadaka yake.
Taswira wakati Ibada Ikiendelea.
Pichani ni sehemu ya Wadau wanajumuiya ya Kyazi-Kahororo.
Mwisho Roho Mtakatifu awaongoze kwenye umoja na ukweli mkamilifu katika kuyatekeleza majukumu ya kila siku