SKYLIGHT BAND NDIO HABARI YA MUJINI KWA SASA, KARIBU THAI VILLAGE TUSEBENEKE PAMOJA LEO
Kikosi kazi cha Skylight Band kikiwajibika jukwaani Ijumaa iliyopita kwenye show zake za kila siku ya Ijumaa ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.....Kutoka kushoto ni Joniko Flower, Aneth Kushaba AK47, Sony Masamba, Mary Lucos na Sam Mapenzi.
Mary Lucos na Hashim Donode wakisebeneka huku Joniko Flower akipiga vocal kwenye show ya aina yake iliyowabamba mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Joniko Flower na Digna Mbepera kwa pamoja wakitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani).
Aneth Kushaba AK 47 akipiga vocal jukwaani.
Kutunza inaruhusiwa hukatazwi ni motisha kwa wanamuziki kama inavyoonekana pichani mdau baada ya kuguswa na burudani ya Skylight Band.
Muddy Bawaziri naye alichomoa bulungutu lake la mijihela na kwenda kuwatunza waimbaji wa Skylight Band.
Uzee mwisho Chalinze mjini kila mtu HONEYYYY..! Babu wa kizungu naye alikuja kusebeneka na Skylight Band kama anayoonekana pichani.
Mashabiki wakichizika na Skylight Band.
Mmoja wa shabiki wa Skylight Band aliyeamua kuvua shati na kubaki na vesti baada ya kukolewa na burudani.
Aneth Kushaba AK (aliyeipa mgongo camera) akionyeshana ufundi na shabiki wa Skylight Band kwenye dancing floor Ijumaa iliyopita ndani kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Shabiki akicheza huku akiwa ameshikilia vinywaji vyake baridi hii yote ni kuepuka kuikosa raha ya muziki kwenye dancing floor na kuamua kuwa karibu na vinywaji vyake.
Kikuweli hawa jamaa pichani ni #Balsaa na hii yote ni kutokana na muziki safi ulioenda shule unaopigwa na Skylight Band. #FullKusebeka
Hashim Donode akipiga vocal huku jukwaani akisindikizwa na Aneth Kushaba AK 47 na Joniko Flower.
Mary Lucos akiwaduarisha mashabiki wa Skylight Band na mambo ya pwani.
Sehemu ya umati wa mashabiki wa Skylight Band wakiduarika Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Mary Lucos akizungusha nyonga...!
Nyomi ya mashabiki wa Skylight Band ikiendelea kula bata Thai Village Ijumaa iliyopita.
I’m looking for my johnny....I’m looking for my honey…ya ya ya....Si mwingine ni Le Manager her self Aneth Kushaba AK47 akiimba wimbo wa Yemi Alade unaokubalika na wengi katika chati za muziki hivi sasa.
Sam Mapenzi akiwajibika jukwaani zile fleva zote za Ki-nigeria utazipata hapo, tukutane baadae ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.