BALOZI KAMALA AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA KAMPUNI YA DELANOUT YA UBELGIJI
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye miwani)
akimkabidhi zawadi ya mwamvuli unaotangaza vivutio vya Utalii Tanzania
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya DELANOUT ya Ubelgiji Bwana. Jackson
Delanout. Balozi Kamala yuko kwenye ziara ya kuhamasisha makampuni ya
Ubelgiji kushiriki kwenye ziara ya biashara ya makampuni ya Ubelgiji
itakayofanyika Tanzania, Novemba mwaka huu.