BALOZI KAMALA AKUTANA NA SENETA WA KWANZA MWAFRIKA KATIKA BARAZA LA SENETI YA UBELGIJI
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kushoto)
akimkabidhi Seneta wa kwanza Mwafrika katika Baraza la Seneti la
Ubelgiji Mhe. Bertin Mampaka. Seneta Mampaka vilevile ni Spika wa Bunge
la Brussels na pia ni Mbunge wa Bunge la Walonia la Ubelgiji. Balozi
Kamala amemuomba Seneta Mampaka kuitangaza vizuri Tanzania katika Baraza
la Seneti la Ubelgiji, Bunge la Brussels na katika Bunge la Walonia.
Aidha, Balozi Kamala amemuomba seneta huyo kuhimiza makampuni mbalimbali
ya Ubelgiji kuwekeza Tanzania. Balozi Kamala yuko kwenye ziara ya
kikazi ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Ubelgiji na kukutana pia na
viongozi mbalimbali wenye ushawishi katika masuala ya Kitaifa,
Kimataifa na Jumuiya ya Ulaya.