Bukobawadau

CAMERA YETU NA UJIO WA MDAU KATARUGA

Uwanja wa Ndege  Mjini Bukoba ni majira ya Saa  3:45 Asubuhi Ndege ya Shirika la ndege la Auric Air inawasili ikitokea Jijini Mwanza.
 Anaonekana Uwanjani hapa Ndugu AbdulRahym Kabyemela  akizungumza kwa simu.
Hawa ni Dereva Tax maarufu wa maeneo Airport
 Ndugu Thomas Charles simu ikiwa sikioni akimpigia pahala.
 Ndugu Al Amini na mwenzake AbdulRahym Kabyemela  wakiwa uwanja wa ndege kumpokea rafiki yao Ben Kataruga.
Watu mbalimbali na Madreva Tax wakichungulia Uwanjani kwa mbali.
Ndege ya Auric ikiwa inawasili.
 Jamaa wakisubilia  abiria.
 Mr. Ben Kataruga anasalimiana na Mr Shumbu.
Mmojawa wa abiria aliyeshuka ndani ya Ndege ya Auric air ni Mr. Ben Kataruga pichani.
 Mr. Ben Kataruga analakiwa na rafiki yake Mr.AbdulRahym Kabyemela
 Wanasalimiana  na kuanza kudasisi ya kwao machache.
 Mdau Al Amin Abdul Amini, Ndugu Thomas ,Mr.AbdulRahym Kabyemela na Mr Ben Kataruga na Timu nzima ya Bukobawadau  wote ni marafiki wakubwa, na Sote ni watu wa watu na tupo hapa kumpokea  Ben Kataruga ambaye ni mtu anayejihusisha kwenye  maswala ya watu wengine wengi.
 Vicheko vya hapa na pale hii na baada ya Mtu kuuliza ;'Imekuwaje leo Mr Kasibila haonekana Air port.'
Mdau Bin Self akiwa na simu sikioni.
 Anaongea na Simu moja Mr.Ben Kataruga ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Ben Expeditions
 Kwa kutumia Kipandio alichojaliwa Ndg Al Amin, wanaongozana kuelekea kunako husika.
Mtu na Swahiba wake wanafika eneo la maegesho ya Victorious Perch Hotel - Bukoba
 Taswira  ya Sehemu ya Maraha Linas Night Club iliyopo barabara ya Uganda mkabala na Victorious Perch Hotel - Bukoba
 Wanabadilishana mawazo kuhusu kuhusu mchakato wa kuelekea Msibani Kijijini Bugandika.
Kama alivyoshauriwa  na Daktari wake wa Afya na maswala ya lishe , anaonekana  Ndg Al Amin akinywa chai pamoja na asali.
 Msosi Victorious Perch Hotel - Bukoba ambapo walipata 'Koleksheni' ya samaki, kuku masala.
 Wakiwa hotelini hapo akawasili Mr Cathbert Basibila pichani katikati.
 Barabarani  nje ya Victorious Perch Hotel  camera yetu Uso kwa uso na Mdau pichani.
 Viunga vya mji wa Bukoba ,muda mchache kabla ya kuelekea Kijijini Bugandika.
 Majengo ya Ushirika  Bugandika.
"Uncle Tom" On Air
  Kijijini Bukandika Sep 17,2014  kushiriki mazishi ya Bi Leokadia Nyamwiza Bujende
 Amoud Migeyo Diwani kata Bugandika Missenyi
 Mmoja wa wafiwa na Sehemu ya Waombolezaji waliofika msibani hapo
Katika hili na lile kama kawaida kwa  mtu wa watu Ben Kataruga.
Pichani ni Mama Mzazi wa Ben Kataruga.
Kanisa la  RC Kijijini Bugandika Missenyi
Kijijini Bugandika tunasema 'kikwetu kwetu' au 'Sambaza upendo Tanzania at 50.
 Amushenye njia ya kuelekea Bugandika ikiwani ni umbali  wa 2.5 miles au 4 KM (kilometers)
Njia panda iliyopo Amushenye Bugandika kwa mbali linaonekana Ziwa Ikimba.
Jioni ya Siku Ndugu Ben Kataruga anakutana na  Mdau Divo maarufu kwa jina la Serikali
 Wakiendelea kubadirishana mawazo na kufurahia siku kwa pamoja
 Muhungwana  pichani ni Mdau Bushila kama kawaida  mtu wa watu
 Mikakati ya hapa na pale ikiendelea wakiwa Prince Hotel-Bukoba
Kuelekea kutoa Salaam meza ya Omlangira Deo Lugaibula na Mzee Kelvin wa Space Motel.
Upande wa pili Mr. Basibila akiendelea  kupata kitu 'Mchemsho wa Ndizi Kwa samaki'
 Mlangira Deo Lugaibula  akiendeleza kumkarimu Mdau Ben Kataruga kwa maneno yake ya ucheshi na uchangamfu.
Mchana wa Jana Sept 18,2014Muonekano wa mandhari nzuri ,taswira sehemu ya Mji wa Bukoba ,na kingo za Ziwa Viktoria.
Hapa ni katikati ya kitovu cha Kilima cha Kashura, ndivyo anavyo onekana Mr Ben Kataruga
akishuhudia taswira ya mji wa Bukoba,muonekano wake wa asili huku ukifurahia upepo mwanana toka ziwani Victoria.

Mr Basibila na Mr Shumbu wakiungana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Ben Expeditions katika sera ya  kudumisha utalii wa ndani....
Hii ni moja kati ya picha
Moja ya mjengo wenye muonekano wa wa kipekee, muonekano wa Kifalme 'Ekikale' iliyopo katikati ya kilima cha Kashura.
Hapa ni Masikani kwa Mdau wetu,mtu wa Watu Ndugu Rady Rweyemamu
Hakika ni nyumba bora ya kisasa na yenye kuvutia ikiwa na Vigezo vyote .
Picha ya kwanza na ya pili ni muonekano wa mandhari nzuri ,taswira sehemu ya Mji wa Bukoba ,na kingo za Ziwa Viktoria.
The View over Lake Victoria
Moja ya Stori kubwa Mjini Bukoba ni Nyumba hii iliyopo eneo la kashura iliyonunuliwa kwa thamani kubwa na kubomolewa Mzee Mwandiki
 Ujenzi ukiendelea upya baada ya nyumba iliyonunuliwa kisha ikabomolewa na  Mzee Mwandiki
 Uso kwa uso na Best advocate Stephen Byabato .
Wakili mahiri (Adv Stephen Byabato)pichani kushoto akiteta jambo na rafiki yake Mr. Ben Kataruga ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Ben Expeditions
Blogger Mc Baraka (pichani kushoto)akifurahia jambo na Mr.Ben Kataruga baada ya kumjulisha  na kumuonyesha  hali halisi juu ya kinachoendelea Mji wa Bukoba.
 Credit Blogger Mc Baraka kuwa sehemu ya vuguvugu na Changamoto Mkoani Kagera
Next Post Previous Post
Bukobawadau