KAMPUNI YA UBELGIJI YA TPF SAMBRE YAANZA KUFANYA KAZI TANZANIA
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (wa pili kutoka
kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa kampuni ya
ushauri ya TPF Basse Sambre baada kukutana nao leo ofisini kwake
Brussels. Wa kwanza kulia ni Bwana. Stefan Pousset Mtendaji Mkuu wa
Kampuni hiyo na wa kwanza kushoto ni Bwana Jerome Bestgen Meneja wa
mauzo wa kampuni hiyo. Wa pili kulia ni Bwana Nyamtara Mukome afisa
katika Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji. Wawakilshi hao walimweleza Balozi
Kamala kwamba wamepata shughuli za kufanya Tanzania na wanatarajia
kufungua ofisi zao Tanzania. Balozi Kamala aliwashauri watafute
Watanzania wa kushirikiana nao ili kampuni yao iweze kuimarika,
kuhimili ushindani katika sekta ya ushauri, kutoa ajira na kusaidia
kujenga uchumi wa Tanzania.