MAJAMBAZI YAVAMIA KITUO CHA POLISI NA KUUA WILAYANI BUKOMBE
Watu wanaosadikika kuwa ni majambazi wamevamia kituo cha polisi
wilaya ya bukombe na kuua askali polisi wawili na kujeruhi askali
wengine wawili.
Akizungumza na waandishi wa habari, mkuu wa jeshi la polisi Igp
Ernest Mangu amesema majambazi hao walivamia kituoni hapo saa nane usiku
ambapo walirusha mabomu na kuua askali wawili, waliouwawa ni wp 7106
Uria Mwandiga na g 2615 Dastani Kimati waliojeruhiwa ni h627 Mohamedi
Hassani na cpl 5131 David Ngupama.
Igp Mangu amesema katika uvamizi huo silaha mbalimbali zimeibiwa
ambapo jeshi la polisi limetangaza zawadi ya shilingi millioni kumi kwa
yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa wahalifu hao na silaha
zilizoibiwa.
Akithibitisha kupokelewa kwa majeruhi na miili ya marehemu mganga
mkuu wa hospitali ya wilaya ya Bukombe daktari Honaratha Rutatinsibwa
amesema hali za majeruhi ni mbaya na wamehamishiwa katika hospitali ya
rufaa Bugando.