MAMBO10 YALIYOTIKISA BUNGE LA KATIBA
Hakuna marefu yasiyo kuwa na ncha, ni usemi wa zamani wa wahenga
wenye maana ya kila jambo lenye mwanzo, lazima litakuwa na mwisho.
Ndivyo ilivyo kwa Bunge la Katiba ambalo safari
yake ilianzia Februari 18 mwaka huu na kutarajia kuhitimishwa Oktoba 4
kwa ajili ya kutoa Katiba inayopendekezwa.
Yapo mengi yaliyofanyika ndani ya Bunge hilo
yakiwamo mazuri yaliyofurahisha masikioni mwa watu, licha ya kuwa kuna
baadhi ya mambo yaliyotoa tafsiri hasi kwa makundi yote.
Mbali ya hayo, ziko ndimi ambazo zilipasua Bunge
hilo na hata wakati mwingine kusababisha mivutano mikali kiasi cha
kuleta mkanganyiko uliotafsiriwa kivingine.
Kikubwa ni kuwa, sasa mchakato huo unafikia mwisho
ili ipatikane Katiba inayopendekezwa ambayo itawekwa kabatini ikisubiri
rais ajaye ambaye ataanzia kura ya maoni kwa wananchi baada ya utawala
wa Rais Jakaya Kikwete.
Mjadala wa Bunge hilo ulitikiswa na mengi lakini kumi ndiyo hasa yalionekana wazi kuleta mvutano mkali kiasi cha kuligawa Bunge hilo ikiwamo suala la kura ya wazi au kura ya siri.
Mjadala wa Bunge hilo ulitikiswa na mengi lakini kumi ndiyo hasa yalionekana wazi kuleta mvutano mkali kiasi cha kuligawa Bunge hilo ikiwamo suala la kura ya wazi au kura ya siri.
Jambo hilo liliibuka katika hatua ya awali ya
kutunga Kanuni zitakazoongoza Bunge hilo. Hofu ya wajumbe ilikuwa kama
kura zingepigwa kwa wazi, kungeibuka hofu kutoka kwa baadhi ya wajumbe
ambao wangeogopa kusurubiwa na vyama vyao au makundi waliyotoka
kushughulikia kama wataenda kinyume na matakwa ya vyama au makundi hayo.
Hata hivyo hali ilikuwa kinyume katika hitimisho,
baada ya wajumbe hao waliokuwa wakitaka kura ya siri kugeuka na kupiga
kura ya wazi licha ya kuwa uhuru ulitolewa wa aina mbili za kura.
Jambo la pili lililochomoza ni suala la uraia
pacha. Hapa palichimbika. wajumbe wote walionyesha umahiri wa kuzungumza
na kujenga hoja wakitaka kuungwa mkono. Kadari Singo ni Mjumbe
aliyeingia katika Bunge hilo akiwakilisha kundi la watu wanaoishi nje ya
nchi (Diaspora), alisimama kidete kulilia haki ya urais pacha ambayo
ilionekana kuwagusa watu wengine ambao walikuwa wakimuunga mkono, huku
hoja mbalimbali zikijengwa kwa ajili ya kutetea jambo hilo.
Lakini mwishowe suala hilo lilipingwa kwa sehemu
kubwa na watawala ambao wamelijengea shaka licha ya kuwa baadhi yao
ndiyo wenye ndugu na watoto walio nje ya nchi.
Katika hatua nyingine, hekima ya Mwenyekiti wa
Bunge hilo Samuel Sitta ilitumika kuzima suala la Mahakama ya Kadhi
ambalo liliibuliwa na watu wa imani ya Kiislamu.
Mbunge aliyewasha moto huo alikuwa Mtutura Abdalah
Mtutura ambaye katika mchango wake aliwahamasisha waumini wa dini ya
Kiislamu kutokuunga mkono Katiba kama haitakuwa na sura ya Mahakama ya
Kadhi. Nalo liliishia kwa mbunge huyo kuomba msamaha na Sitta
kulisawazisha kwa kutoa ahadi ya kuliweka katika mfumo mzuri ndani ya
Katiba.
Jambo la nne lililotikisa ni wajumbe wenye mamlaka kupinga
Rasimu ya Katiba katika kipengele cha wabunge kuwa mawaziri. Waziri wa
Elimu Dk Shukuru Kawambwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Profesa Anna Tibaijuka walipinga hoja hiyo.
Viongozi hao walizungumza kwa mifano namna
inavyokuwa ngumu kwa waziri ambaye ni mbunge kutekeleza majukumu yake.
Wanasema anakosa muda wa kuwatumikia wapiga kura wake kikamilifu.
Mjadala huo pia ulikolezwa na suala la kiwango cha
elimu kwa mbunge. Licha ya Tanzania kuwa na utitiri wa shule za
Sekondari, mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde, aliongoza hoja ya kutaka
sifa ya kugombea nafasi za kisiasa ibaki kuwa ni kujua kusoma na
kuandika.
Ilikuwa kama masihara lakini mwakilishi huyo
alijenga hoja ambayo ilionekana kuungwa mkono na watu wengi huku wengine
wakipinga. Naibu Waziri wa Ujenzi Gerson Lwenge ni miongoni mwa wajumbe
waliopinga hoja hiyo.
Suala la muungano nalo lilivuta hisia kali hasa
katika kipengele cha nafasi ya Rais, Makamu na Waziri Mkuu. Hapa
wajumabe walijikuta wakikwepa mvua na kukanyaga umande. Rasimu
ilipendekeza Serikali tatu ambazo zingekuwa na marais watatu, lakini wao
wakapigia chapuo Serikali mbili zenye rais wawili na Makamu watatu.
Pendekezo la walio wengi ni kuwepo kwa rais wa Muungano, Makamu wake, rais wa Zanzibar kuwa Makamu na Waziri Mkuu kuwa katika nafasi ya umakamu pia kama ilivyo mwanzo kabla ya mfumo wa vyama vingi. Wanawake kwa upande wao walionekana kujipanga zaidi katika usawa wa kijinsia kwenye uongozi kutoka ngazi ya chini hadi juu. Jambo hilo lilileta msuguano wa uelewa lakini mwisho lilihitimishwa kwa wengi kulikubali.
Pendekezo la walio wengi ni kuwepo kwa rais wa Muungano, Makamu wake, rais wa Zanzibar kuwa Makamu na Waziri Mkuu kuwa katika nafasi ya umakamu pia kama ilivyo mwanzo kabla ya mfumo wa vyama vingi. Wanawake kwa upande wao walionekana kujipanga zaidi katika usawa wa kijinsia kwenye uongozi kutoka ngazi ya chini hadi juu. Jambo hilo lilileta msuguano wa uelewa lakini mwisho lilihitimishwa kwa wengi kulikubali.
Pia kulikuwa na hoja ya wabunge kuwajibishwa na
wananchi pale wanaposhindwa kuwajibika ipasavyo. Hapa Bunge
liligawanyika kati ya wajumbe wa kundi la 201 na wale ambao wanatoka
katika Bunge la Muungano na Baraza la Wawakilishi.
Kundi la 201 walitaka kipengele hicho kibaki wakati wengine wakitaka kiondolewe kabisa.
Hoja nyingine ikawa ni suala la mfuko wa pamoja na
hadhi ya Zanzibar katika masuala mazima ya fedha ikiwamo kilio cha
kutaka mgao wa fedha za misaada ziongezwe katika upande huo wa pili wa
Muungano badala ya kile cha sasa cha asilimia 4.5.
Pamoja na wote kujitahidi kuliweka sawa jambo
hilo, Mbunge wa Nkasi Kaskazini Alli Keissy Mohamed alitibua mambo,
baada ya kueleza kuwa Wazanzibari hawana kitu na kwamba wanaishi kwa
fadhila za Tanganyika.
Nusura ngumi zipigwe ndani ya ukumbi wa Bunge hilo
na kama si watu wa usalama kusimama kidete, huenda mambo yangeharibika,
kwani kila mmoja alionyesha kuchukizwa na maneno ya mbunge huyo ambaye
tangu wakati huo hadi sasa anasimamia msimamo wa Serikali tatu ili
kuwepo na hali ya kila mmoja kuwajibika.
MWANANCHI.
MWANANCHI.