MSANII METTY KUZINDUA WIMBO WAKE MPYA "NAJUA" JUMATANO HII
Wimbo
mpya ya msanii Metty iitwayo "Najua" inatarajiwa kuzinduliwa tarehe 1
Octoba siku ya jumatano ya wiki hii katika vyombo mbalimbali vya habari
ndani na nje ya Tanzania.
Wimbo
huo amashirikishwa msanii Conrad anaekuja kwa kasi katika tasnia ya
muziki wa bongo flava ikiwa wapenzi wengi wa muziki wa kizazi kipya
watapata nafasi ya kumfahamu msanii huyo.
Najua ni wimbo uliotayarishwa katika studio mpya za kisasa Centric Records chini ya producer Eng.Davy Machords.
Metty amewaomba wadau na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya kutoa ushirikiano wa nguvu katika kazi zake za muziki.