NBS YASISITIZA MATUMIZI YA KANZA YA TAKWIMU ZA KILIMO
Mkuu wa
Idara ya Utawala na Rasilimali wa ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Gabriel Madebe akifungua
semina ya wadau ya uhamasishaji wa
matumizi takwimu za kilimo zinazopatikana kupitia Kanzi rasmi ya takwimu za
kilimo inayopatikana katika anwani ya
Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya www.nbs.go.tz leo jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Bi. Julia Stone akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa semina ya uhamasishaji wa matumizi ya Kanzi ya takwimu za Kilimo nchini leo jijini Dar es salaam.
Mratibu wa Kanza ya Takwimu za Kilimo Tanzania Bw. Basike Mteleka akijibu maswali ya wadau mbalimbali waliohudhuria semina ya uhamasishaji wa matumizi ya Kanzi ya takwimu za Kilimo nchini .
Wadau mbalimbali waliohudhuria semina ya uhamasishaji wa matumizi ya Kanzi ya takwimu za Kilimo nchini Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa semina hiyo leo jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Bi. Julia Stone akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa semina ya uhamasishaji wa matumizi ya Kanzi ya takwimu za Kilimo nchini leo jijini Dar es salaam.
Mratibu wa Kanza ya Takwimu za Kilimo Tanzania Bw. Basike Mteleka akijibu maswali ya wadau mbalimbali waliohudhuria semina ya uhamasishaji wa matumizi ya Kanzi ya takwimu za Kilimo nchini .
Wadau mbalimbali waliohudhuria semina ya uhamasishaji wa matumizi ya Kanzi ya takwimu za Kilimo nchini Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa semina hiyo leo jijini Dar es salaam.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
26/9/2014, Dar es salaam.
Ofisi ya Taifa ya
Takwimu imewataka watunga Sera, taasisi,
mashirika, na wadau mbalimbali wa
maendeleo kuitumia Kanza (Data base) rasmi ya takwimu za Chakula na Kilimo iliyoanzishwa
hapa nchini kwa lengo la kutoa takwimu za
Kilimo kutoka katika maeneo mbalimbali.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakati wa ufunguzi wa semina ya kuhamasisha matumizi
ya Kanza hiyo leo jijini Dar es salaam, Mkuu
wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu wa
ofisi hiyo Bw. Gabriel Madembwe amesema upatikanaji wa taarifa za sekta ya
Kilimo na Chakula kutoka katika maeneo mbalimbali ya uzalishaji hapa nchini umerahisishwa
kupitia Kanza hiyo inayopatikana kupitia
tovuti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya www.nbs.go.tz
Amesema takwimu zilizo
katika Kanza hiyo zitaiwezesha serikali, watunga sera na wadau mbalimbali wa
maendeleo wa ndani na nje ya nchi kufanya maamuzi sahihi wakati wa kupanga mipango
ya maendeleo kwa wananchi na kutatua
changamoto mbalimbali zinazokabili sekta ya kilimo nchini.
Amesema matumizi ya
Kanza hiyo yanawarahisishia wadau hao kupata taarifa za Kilimo na chakula kwa
urahisi zilizokusanywa kutoka katika taasisi
mbalimbali na wizara zinazohusika na sekta ya Kilimo hapa nchini.
Amesema matumizi Kanza hiyo yataondoa hali iliyokuwepo
hapo awali ya ugumu wa upatikanaji wa
takwimu kutokana na mtawanyiko wa takwimu hizo na kuwataka wadau wote wa sekta hiyo walio katika ngazi ya maamuzi
kuielewa na kutumia.
Amefafanua kuwa takwimu zinazowekwa katika Kanza hiyo zinahusu
Kilimo, Uvuvi, Biashara, Uzalishaji na upatikanaji wa chakula katika mikoa
mbalimbali ya Tanzania na kuongeza kuwa kazi ya uwekaji na uhuishaji wa takwimu hizo inafanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa
ushirikiano wa wataalam kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Viwanda na Biashara.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sera na Mipango, Wizara ya Kilimo, Chakula na
Ushirika Bw. Oswald Luboha akitoa ufafanuzi kuhusu Kanzi hiyo amesema ilianzishwa mwaka 2005 na
kuzinduliwa rasmi mwaka 2012 kwa lengo la kuweka pamoja takwimu za kilimo ili
wadau wa sekta ya Kilimo waweze kuzipata kwa urahisi.
Amesema Tanzania ina
maeneo mengi yanayofaa kwa uzalishaji kwa
shughuli za kilimo hivyo kuna umuhimu wa maeneo hayo kujulikana, ukubwa wake na
mazao yanayolimwa katika maeneo hayo
Amesema Tanzania
inafanya vizuri kwa kufanya sensa ya Kilimo kila baada ya miaka 5 ikilinganishwa
na nchi nyingine za Afrika ya Mashariki hivyo kupunguza muda wa kufanya sensa ya kilimo kutoka miaka
10 iliyoainishwa na Shirika la Chakula Duniani (FAO).
Naye mwakilishi wa
Shirika la Chakula Duniani (FAO) Bi. Julia Stone akizungumza katika semina hiyo
ya uhamasishaji amesema kuwa Tanzania
inafanya vizuri katika kuhakikisha kuwa takwimu sahihi za kilimo zinapatikana
kutokana na ushirikiano uliopo wa wizara husika na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
Kuhusu mchango wa FAO
katika kufanikisha tafiti mbalimbali zinazoendelea hapa nchini amesema Tanzania
itaendelea kunufaika kutokana na kuwa miongoni mwa nchi 17 za Afrika
zinazoshirikiana na Shirika la Chakula Duniani (FAO) kupitia taasisi ya Bill na
Melinda Gates.
MWISHO