NGOMA AFRICA BAND YAITAKIA MSONDO NGOMA BAND HERI YA MIAKA 50
Msondo Ngoma Band kutimiza miaka 50 mwezi Oktoba 2014, Ras Makunja ameitaja Msondo ndio bendi pekee kongwe Afrika !
Bendi maaru ya muziki wa dansi barani
ulaya Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni almarufu pia kama viumbe wa
ajabu Anunnaki Aliens wenye makao nchi Ujerumani. bendi hiyo inapeleka
salam za kuitakia heri ya miaka 50 bendi kongwe barani afrika MSONDO
NGOMA MUSIC BAND aka Baba ya Muziki ya watanzania ambayo mwezi Oktoba
2014 itatimiza miaka 50 na kuweka rekodi ya kuwa bendi kongwe pekee
barani Afrika !
Kiongozi wa Ngoma Africa band Kamanda
Ras Makunja,maitaja bendi ya Msondo Ngoma ndiyo bendi pekee kongwe
inayoendelea kutamba tatika medani ya muziki wa dansi barani Afrika na
watanzania tuna haki ya kujivunia,
Makunja alisema
Msondo Ngoma ilianzisha 1964 kama NUTA Jazz,baadaye kubadili majina kama
JUWATA (OTTU) kutoka na wamiliki wa mwanzo Jumuiya ya wafanyakazi
Tanzania kubadili majina, na sasa Msondo Ngoma Band aka Baba ya Muziki,
kweli ni Baba ya Muziki,maana hakuna bendi kongwe Afrika zaidi ya
Msondo, mfano bendi kongwe kama Orch.Baobab ya Senegal ilianzishwa 1970
haiwezi kuwa kongwe! Zaiko Langa langa (DRC) ilianzishwa 1969 haiwezi
kuwa kongwe mbele ya Msondo Ngoma, na T.P OK
jazz ya marehem Franko wa DRC ndio ilikuwa kongwe ilianza 1956 sasa haipo tena,kuna bendi ya Bana Ok ! ya Lutumba Simaroo.
Ras
Makunja alisema Msondo Ngoma band ni ya watanzania lazima tujivunie
Hongereni sana ! baba ya muziki Msondo Ngoma band kwa kuelekea kutimiza
miaka 50.