PAPA FRANCIS AMEMFUTA KAZI ASKOFU ROGELIO
Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, amemfuta kazi Askofu
Rogelio Livieres Plano wa Paraguay kwa kile kilichoelezwa na Vatican
kwamba ni kitendo cha askofu huyo kumlinda padri anayetuhumiwa
kuwadhalilisha kingono watoto wadogo.
Ujumbe kutoka Vatican ulikuwa umetumwa nchini Paraguay kuchunguza tuhuma kwamba askofu huyo alikuwa akimpandisha daraja na kumtetea padri huyo raia wa Argentina.
Ujumbe kutoka Vatican ulikuwa umetumwa nchini Paraguay kuchunguza tuhuma kwamba askofu huyo alikuwa akimpandisha daraja na kumtetea padri huyo raia wa Argentina.