SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LAWAWEZESHA VIJANA MKOANI KAGERA KUJIAJILI KUPITA MASHINE ZA KUFYATUA TOFALI ZA GHARAMA NAFUU
Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) lawawezesha vijana Mkoani Kagera kujiajili kwa kuwapatia mashine 32 za
kisasa za kufyatua matofali yenye gharama nafuu zenye jumla ya gharama ya
shilingi 14,400,000/=
Mashine hizo zilikabidhiwa
kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe ofisini kwake kwenye
hafla fupi na mwakilishi wa shirika la Nyumba la Taifa Bw.Adrian Dominick tarehe 1, 2014.
Mashine za tofali nafuu.
Katika hafla hiyo Mkuu wa
mkoa alizikabidhi mashine hizo kwa Wakurugenzi na Wenyeviti wa Halmashauri nane
za Mkoa wa Kagera kwajili ya kuzikabidhi mashine hizo kwenye vikundi vya vijana
katika halmashauri zao.
Akikabidhi Mashine hizo Bw.
Adrian kwa Mkuu wa Mkoa alisema dhumuni kubwa la shirika ni kuwawezesha vijana
kujiajili na kutoka vijiweni ili kujiunga katika vikundi na kufanya kazi kwa
kujituma na kujiingizia kipato halali.
Aidha Bw. Adrian alisema
mashine hizo zitawasaidia wananchi wa Mkoa wa Kagera kujenga nyumba za gharama
nafuu kwa kutumia matofali yanayoingiliana bila kutumia udongo yatakayofyatuliwa
kwa kutumia mashine hizo za kisasa.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera
akikabidhi mashine hizo kwa Halmashauri za Wilaya alisema ili kuhakikisha
vijana wanajiajili sasa ni wakati taasisi za serikali na wananchi binafsi
kuanza kutumia matofali yatakayozalishwa kwenye vikundi hivyo vya vijana ili
kuwapa vijana ajira.
Aidha alilishukuru Shirika
la Nyumba la Taifa kuukumbuka Mkoa wa Kagera katika kupunguza tatizo la ajira
kwa vijana, pia aliwaasa vijana kujituma na kuchapa kazi kwa bidii ili kupata
maisha bora.
Kila Halmashauri ya Wilaya
ilipewa mashine nne aidha kikundi kitakachonufaika na mashine hizo pia
kitawezeshwa shilingi 500,000/= na shirika la Nyumba la Taifa kama mtaji wa kuanzia uzalishaji wa tofali
zenye gharama nafuu.