SHUKRANI YA MSIBA WA BI STEPHANIA J.KAGANDA
Bw.
Deusdedit B. Kaganda kwa niaba ya familia ya Mzee Boniface Kaganda wa
Dar es Salaam, anapenda kutoa shukrani kwa ndugu, jamaa na marafiki
walioshiriki katika kipindi chote cha kumuuguza na kushiriki shughuli ya
msiba wa Bi. Stephania J. Kaganda, aliyefariki tarehe 12 Agosti na
kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele tarehe 15 Agosti 2014, huko
kijijini Lukindo, Katoma, Bukoba.
Shukrani za
pekee ziwafikie Baba, Mama, Kaka na Dada na watoto wa marehemu kwa
kumuuguza kipindi chote
cha kuugua kwake, Bi. Winnie Max, madaktari na wauguzi wa Hospitali ya
Mkoa wa Kagera. Dr. Ephraim Kato, madaktari na wauguzi wa Hospitali ya
Mgana, Bukoba pamoja na Dr. Jean-Pierre Stamm wa clinic ya Medicine
Generale FMH, Versoix, Geneva, Switzerland.
Shukrani
pia ziwafikie, Majirani na Jumuiya ya Mt. Thomas Acquinas wa Karakata,
Airport, Dar es Salaam, Jumuiya ya Kitagata, Lukindo, Katoma, pamoja na
Paroko wa Parokia ya Katoma, Bukoba kwa kumjali kipindi chote cha kuugua
na kushiriki misa takatifu siku ya msiba.
Shukrani
za dhati ziwafikie Katibu Mkuu na wafanyakazi wa Ofisi ya Rais,
Utumishi wa Umma kwa ushirikiano mkubwa wakati wa kipindi cha kuugua na
msiba, Wafanyakazi wa Ofisi ya Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania,
Geneva, Switzerland pamoja na watanzania wote waishio Uswisi kwa msaada
wa hali na mali kufanikisha shughuli ya msiba.
TULIKUPENDA LAKINI MUNGU AMEKUPENDA
ZAIDI