WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS ILALA 2014 WATAMBULISHWA RASMI KWA MASHABIKI WA SKYLIGHT BAND
Vijana wa Skylight Band wakitoa burudani kwa mashabiki wao huku wakiongozwa na Mary Lucos (kushoto) katika show zao za kila Ijumaa kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar bila kusahau leo pia watakuwepo kuanzia saa tatu usiku.
Kijana Hashim Donode akionyesha hisia kali wakati akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar. Kushoto ni Meneja wa Band Aneth Kushaba akimpa sapoti.
Mashabiki wa Skylight Band wakiburudika na nyimbo mbalimbali zilizokuwa zikiporomoshwa na bendi hiyo.
Meneja mwenyewe huyo Aneth Kushaba AK 47 akipiga vocal kwa hisia kali kabisa kuhakikisha mashabiki wa Skylight Band roho zao zinasuuzika.
Sony Masamba a.k.a Fally Ipupa wa Bongo akifanya yake jukwaani huku kushoto na kulia akisindikizwa na Aneth Kushaba AK47 na Mary Lucos.
Pichani juu na chini ni washiriki wa shindano la Miss Ilala 2014 litakalofanyika Jumamosi hii ndani ya hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro wakitambulishwa mbele ya mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Washiriki wa shindano la Miss Ilala 2014 wakijimwaga uwanjani na burudani ya Skylight Band ndani kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar Ijumaa iliyopita.
Pichani juu na chini ni walimbwende wa shindano la Miss Ilala 2014 wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kutambulishwa rasmi kwa mashabiki wa Skylight Band ambapo Jumamosi hii atapatikana mshindi wa taji hilo ndani ya Hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro jijini Dar.
Mary Lucos akiwaduarisha mashabiki wa Skylight Band kwa hisia kali Ijumaa iliyopita kwenye viunga vya Thai Village Masaki jijini Dar.
Umati wa mashabiki wa Skylight Band wakiduarika kwa raha zao na burudani kutoka kwa Mary Lucos (hayupo pichani).
Nyomi ya kufa mtu ni matumaini yangu ya leo itakuwa zaidi ya jana....Karibuni wote mjiachie na Skylight Band ndio habari ya mujini.
Sam Mapenzi akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye viunga vya Thai Village Masaki jijini Dar.
Mashabiki wanaruhusiwa kuja kusheherekea siku zao za kuzaliwa na Skylight Band pamoja na zawadi ya kuimbiwa kama wanavyoonekana pichani wadau kutoka Startimes.
Birthday girl kutoka Startimes akipetiwa petiwa na marafiki zake waliojumuika nae kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.
Walimbwende wakiendelea kula bata ndani ya kiota cha Thai Village huku burudani ikiendelea ya Skylight Band.
William Malecela a.k.a LEMUTUZ akishow love na Mama Chicago.
LEMUTUZ akiwa na familia ya Chicago Ma-telephone.
Rais wa Wanamanyoya Justine Ndege akipata ukodak na kijana wake Mary Lucos wa Skylight Band.
Rais wa Wanamanyiya Justine Ndege akipata ukodak na vijana wake kushoto ni Hashim Donode na Tophy Bass wa Skylight Band.
Rais wa Wanamanyiya Justine Ndege akipata ukodak na wadau wa shindano la Miss Ilala 2014 linalotarajia kufanyika Jumamosi hii ndani ya hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro.
#MahabaNiuwe# Emma Bass wa Skylight Band akishow love na waubavu wake.
Wanamanyoya wakiwakilisha vilivyo kwa ukodak.